Home Mchanganyiko RAIS SAMIA SULUHU AMPENDEKEZA DK.PHILIP MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS

RAIS SAMIA SULUHU AMPENDEKEZA DK.PHILIP MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS

0

Na.Alex Sonna,Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philiph Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jina la Dkt. Mpango limesomwa bungeni jijini Dodoma leo  Machi 30, 2021 na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa kiongozi mkuu huyo wa nchi.
 Spika Ndugai ameanza kusoma nyaraka hiyo ya Mhe. Rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina ambapo
baada ya kusoma jina wabunge walishangilia kwa nguvu.
Wakati hayo yakiendelea Dkt. Mpango alionekana kushikwa na butwaa huku wabunge wakinyanyuka kwenye viti vyao na kumfuata kumpongeza kisha Dkt. Mpango akasimama kuzungumza akishukuru kwa pendekezo hilo huku akielezea pia historia yake.

Sasa Bunge linaanza mchakato wa kuthibitisha jina hilo ambapo Wabunge watapaswa kulithibitisha kwa zaidi ya 50% ya kura za Wabunge wote.