Home Mchanganyiko HAYATI MAGUFULI ALIWAJALI WACHIMBAJI WAZAWA

HAYATI MAGUFULI ALIWAJALI WACHIMBAJI WAZAWA

0
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Mirerani
Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Franone Mining Ltd ya machimbo ya madini ya Tanzanite ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Vitus Ndakize amesema watamuenzi Rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli kwani aliwajali wachimbaji wazawa.
Ndakize ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa pole kwa watanzania kwa kifo cha hayati Magufuli ambaye amezikwa jana Wilayani Chato Mkoani Geita.
Amesema hayati Magufuli aliwaamini wachimbaji wazawa kuwa wanaweza na kweli wakaweza kwani wamefanya kazi bila kutegemea wageni.
Ametoa pole kwa wachimbaji madini na watanzania kwa ujumla kwa kuondokewa na kiongozi wao mpendwa hayati Magufuli.
Amesema ili kulinda rasilimali ya madini ya Tanzanite, hayati Magufuli aliagiza ukuta ujengwe na kusababisha kupandisha hadhi madini hayo.
“Hivi sasa wachimbaji madini ya Tanzanite wanachimba madini yao vizuri bila hofu na miundombinu ya barabara ya kwenda migodini imechongwa,” amesema.