Home Mchanganyiko MBUNGE WA KWELA MHE.DEUS SANGU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA HAYATI DK. MAGUFULI...

MBUNGE WA KWELA MHE.DEUS SANGU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA HAYATI DK. MAGUFULI VIWANJA VYA BUNGE

0

MBUNGE wa Jimbo la Kwela Mkoani Rukwa (CCM),Mhe. Deus Sangu,akisaini kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli katika viwanja vya Bunge kabla ya kuwasili kwa mwili wa Hayati Dkt.Magufuli bungeni hapo leo Machi 22,2021 jijini Dodoma.

Buriani Baba, Kwaheri Kiongozi Wetu Kwa heri shujaa wetu, ndivyo anavyoonekana kusema katika moyo wake Mh. Deus Sangu.

Mhe.Sangu  ameungana na wabunge wengine kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli ambaye mwili wake umefikishwa bungeni na wabunge kutoa heshima zao za mwisho.

Mbunge wa jimbo la Kwela Mhe.Deus Sangu amemuelezea Hayati Magufuli kuwa alikuwa kiongozi shupavu aliyeongoza Taifa kwa ujasiri na Uthubutu ambaye alionesha mapenzi yake dhahiri kwa Watanzania.