Home Mchanganyiko WANAFUNZI ILEMELA WAASWA KUZINGATIA USAFI 

WANAFUNZI ILEMELA WAASWA KUZINGATIA USAFI 

0
***************************************
Wanafunzi wa jinsia ya kike wa shule za sekondari ndani ya jimbo la Ilemela wametakiwa kuzingatia usafi wa miili yao haswa wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Bi Fatma Kaloli wakati akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kabuhoro iliyopo kata ya Kirumba zilizotolewa na taasisi ya AGRI Thamani inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la taasisi zisizo za Serikali (NGO) Mhe Neema Lugangira ikiwa ni ishara ya kuunga  mkono juhudi za mbunge wa jimbo hilo Mhe Dkt Angeline Mabula katika kutatua kero na changamoto za sekta ya elimu kwa kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia ambapo amewataka wanafunzi hao kuwa wasafi na kujiamini wanapokuwa katika vipindi vya hedhi 
‘.. Mbunge ameniagiza niwaletee taulo za kike, Anawataka muwe wasafi, Serikali ya Rais Magufuli inatoa elimu bure kupitia nyinyi tutapata akina Angeline Mabula na kina Neema Lugangira wengine ..’  Alisema 
Aidha Katibu huyo akawataka wanafunzi hao kuzingatia elimu badala ya kujiingiza katika mambo yasiyofaa ikiwemo ndoa za utotoni, mimba, ulevi na uasherati kwani Serikali imewekeza rasilimali nyingi kwao na jamii ikiwategemea
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Kabuhoro Mwalimu Fatma Akilimali mbali na kuwashukuru wabunge hao kwa kufanikisha upatikanaji wa taulo hizo kwa wanafunzi wake, ameahidi shule yake kufanya vizuri kitaaluma ili kuwatia moyo viongozi hao sanjari na kuomba wadau wengine kujitokeza ili kuendeleza gurudumu la maendeleo
Nae Kiranja mkuu wa shule hiyo Dorice Jackson akaishukuru taasisi ya AGRI Thamani na Mbunge Mhe Dkt Angeline Mabula kwa msaada walioutoa kwani walikuwepo baadhi ya wanafunzi wanaoshindwa kununua taulo hizo hivyo kuwafanya kutoshiriki kikamilifu katika masomo  sambamba na wengine kuingia katika vishawishi ili waweze kumudu gharama za kupata taulo hizo
Zoezi la ugawaji wa taulo za kike mashuleni litaendelea tena hapo kesho kwa kugawa taulo hizo katika shule mbalimbali za sekondari za ndani ya jimbo hilo.