Home Mchanganyiko TBS KAGERA YAMUENZI JPM KWA KUWAPA MAFUNZO YA UJASILIAMALI WATU WASIO SIKIA...

TBS KAGERA YAMUENZI JPM KWA KUWAPA MAFUNZO YA UJASILIAMALI WATU WASIO SIKIA ILI KUENDELEZA YALE ALIYOYAACHA

0

 …………………………………………………………………………………

Na Silvia Mchuruza,Kagera.

Shirika la viwango Tanzania TBS limetoa mafunzo ya biashara kwa wajasiliamari wanaoishi na ulemavu wa  kusikia wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki na uchakataji wilayani muleba  mkoani Kagera kwa lengo la kuwataka na wao kusajili biashara zao katika shirika hilo.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo ambayo yamejumuisha viongozi mbalimbali wa mkoa na washiriki zaidi ya 60 ndg.Hamis Sudi Mwanasala ambae ni amewata kusajili biashara zao ili shughuri zao ziwe zenye tija kwa jamii..

Hata hivyo nae mgeni rasmi wa mafunzo hayo ambae ni afisa biashara wa mkoa ndg.Isaya Tendega kwa niaba ya naibu waziri wa viwanda mh.Exand Kigahe ( Mb ) amewashukuru TBS kwa kulatibu na kugharamia mafunzo hayo kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya muleba.

Pia amewapongeza TAMBITA ambayo itawasaidia wajasiriamali haokukuza uchumi wao na itawasaidia wazalishaji wa asali muleba na biharamulokulasimisha biashara zao lakini pia amewataka wasajili vikundi vyao hili waweze kufaidika na  asilimia 2 za halmashauri kwa walemavu.

Nae mkuu wa wilaya ya muleba ndg.Richard Ruyango akusita kuwashukuru TBS kwa kuweza kuwaunganisha washiriki na kuwajengea uwezo katika suala la ufugaji wa nyuki.

“Kipo kikundi cha walemavu  kina mizinga 100 ambayo itawasaidia washiriki katika uzalishaji “

Aidha ametoa wito kwa maafisa misitu kuvisaidia vikundi vya walemavu ili viweze kupata maeneo mazuri ya ufugaji katika wilaya ya  muleba na kumwagiza mkurugenzi kukisajili kikundi hicho ili kiweze kupata mkopo na kujiendesha.

Sambamba na hayo nao washiriki wamewashukuru viongozi wa mkoa kwa kutambua mchango wa katika jamii bila kuwasahau TBS  ambao wao walikuwa waandaji wa mafunzo hayo na kuwapa elimu ya kutosha katika kusajili biashara zao.