Home Michezo NAMUNGO FC YAZIDI KUGAWA POINTI KOMBE LA SHIRIKISHO, YACHAPWA 2-0 NA PYRAMIDS...

NAMUNGO FC YAZIDI KUGAWA POINTI KOMBE LA SHIRIKISHO, YACHAPWA 2-0 NA PYRAMIDS YA MISRI UWANJA WA MKAPA

0

MABAO ya Ramadhani Sobhi dakika ya 71 kwa penalti na Omar Gaber dakika ya 84 leo yameipa Pyramids FC ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Pyramids wanaendelea kuongoza kundi baada ya kukusanya pointi zote sita kwenye mechi mbili za awali, kufuatia kuichapa na Nkana FC ya Zambia 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano iliyopita Cairo.
Namungo yenyewe inaendelea kushika mkia baada ya kufungwa pia na Raja Club Athletic Jijini Casablanca 1-0 Jumatano iliyopita.