Home Mchanganyiko JKT KULIMA EKARI 28,000 ZA MAZAO MBALIMBALI IFIKAPO MWAKA 2024/25

JKT KULIMA EKARI 28,000 ZA MAZAO MBALIMBALI IFIKAPO MWAKA 2024/25

0

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kukagua shamba la Mahindi la ekari 1500 linalolimwa na kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa kwa dhumuni la kuzalisha chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT Leo March 17,2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa JKT, Kanali Hassan Mabena,akielezea mazoa  ya kimkakati inayotekelezwa na Jeshi hilo walipokuwa wakikagua  shamba la Mahindi la ekari 1500 linalolimwa na kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa kwa dhumuni la kuzalisha chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT Leo March 17,2021.

Kamanda wa Kikosi 847 KJ cha Milundikwa JKT, Luteni Kanali Philemon Mahenge, amesema katika msimu wa 2020/21 walipewa lengo la kulima ekari 1500 na wamefanikiwa kulitekeleza na kwamba kwenye msimu ujao wanatarajia kulima ekari 2000.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akiangalia Mahindi yaliyolimwa katika shamba la Mahindi la ekari 1500 lna kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa kwa dhumuni la kuzalisha chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT Leo March 17,2021.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge mwenye miwani kushoto,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa JKT, Kanali Hassan Mabena (katikati) wakati walipotembelea  shamba la Mahindi la ekari 1500 linalolimwa na kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa kwa dhumuni la kuzalisha chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT,kulia ni Kamanda wa Kikosi 847 KJ cha Milundikwa JKT, Luteni Kanali Philemon Mahenge Leo March 17,2021.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge Mwenye miwani kushoto akimsikiliza Kamanda wa Kikosi cha 847 KJ Milundikwa JKT,Luteni Kanali Philemon Mahenge walipokuwa wakikagua shamba la Mahindi la ekari 1500 linalolimwa na kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa kwa dhumuni la kuzalisha chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT,(katikati) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa JKT, Kanali Hassan Mabena Leo March 17,2021.

Muonekano wa shamba la Mahindi la ekari 1500 linalolimwa na kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akizindua Ghala la Kuhifadhi Mazao katika kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa  Leo March 17,2021.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge Mwenye miwani ,akifunua kitambaa kuashiri uzinduzi wa Ghala la Kuhifadhi Mazao katika kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa  Leo March 17,2021.

Muonekano wa Ghala la Kuhifadhi Mazao lililopo katika kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa  Leo March 17,2021.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akizungumza na vijana wa JK mara baada ya kuzindua Ghala la Kuhifadhi Mazao katika kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa  Leo March 17,2021.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge akimkabidhi kiasi cha milioni moja Kiongozi wa Vijana Raphael Kanywanga ambayo watanunua ng’ombe kwa ajili ya kufanya sherehe mara baada ya kuwashukuru kwa kazi nzuri ya ujenzi waGhala la Kuhifadhi Mazao katika kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Rukwa  Leo March 17,2021.

…………………………………………………………………………………………..

Na Alex Sonna, Nkasi

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge, amesema ifikapo mwaka 2024/25 jeshi hilo litakuwa na uwezo wa kulima ekari 28,000 za mazao mbalimbali kwenye vikosi vyake ili kujitosheleza kwa chakula na kuondokana na kuitegemea serikali.

Meja Mbuge ameyasema hayo leo March 17,2021 katika Kikosi cha 847 KJ cha Milundikwa wilayani Nkasi Mkoani Rukwa alipokuwa akieleza kilimo cha kimkakati kinachotekelezwa na jeshi hilo.

Amesema kutokana na mikakati iliyowekwa kwenye kilimo ndani ya jeshi hilo ifikapo mwaka huo watakuwa na uwezo wa kulima hekari hizo ambapo kwasasa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2020/21 ekari 12,247 za mazao mbalimbali ikiwamo mpunga na mahindi zimelimwa.

Amebainisha malengo ya JKT ni ifikapo mwaka huo wajitegemee kwa chakula kwa asilimia 100, ili kuipunguzia serikali gharama za kuwahudumia vijana wa JKT na badala yake fedha hizo zitumike kwenye ujenzi wa miundiombinu ya elimu na afya.

“Tunataka ifikapo mwaka 2024/25 tuwe na uwezo wa kulima ekari 28,000 ambazo zitakuwa tayari zinajitosheleza kujilisha ndani ya JKT, na jamii yetu inanufaika kwa mambo mengi kwa mfano Chita kuna maji yalikuwa yanatoka milimani na kuathiri mashamba tumedhibiti kwa kujenga skimu za umwagiliaji na wananchi wameondokana na mafuriko ya mara kwa mara,”amesema

Amesema uzalishaji huo utakapojitosheleza ndani ya jeshi na kuwa na ziada itauzwa kwa wananchi ili jeshi lipate faida zaidi.

“Pia uzalishaji huu tunaenda sambamba na ujenzi wa maghala ya kuhifadhi chakula chetu, kwa hapa kikosi cha Milundikwa tumejenga ghala lenye uwezo wa kuchukua gunia 20,000 hadi 40,000 na Chita tumejenga ghala lenye uwezo wa kuchukua gunia 150,000 hadi 200,000,”amesema.

Mkuu huyo amesema wataendelea kujenga maghala hayo maeneo mbalimbali wanayolima maharage na mahindi.

Awali, amefafanua maono ya jeshi hilo kujitegemea kwa chakula kuwa ni alipoteuliwa na Rais Dk.John Magufuli walikaa na wenzake na kuangalia sekta ambayo itasaidia JKT kusonga mbele na kuona ni sekta ya kilimo.

“Niliunda kamati na tulianza na kilimo cha dharura kwa mwaka 2019/20 katika vikosi viwili ndani ya JKT tukalima ekari 2200, lakini ndani ya JKT kwa ujumla tulilima ekari 8,517, mikakati iliyokuwepo katika kikosi chetu cha Chita 837 KJ Morogoro tulilima hekari 1000 za mpunga, na kikosi cha Milundikwa 847 KJ tulilima mahindi hekari 1000 na maharage hekari 200,”amesema.

Aidha amesema baada ya kilimo cha dharura walianza kilimo cha kimkakati ambapo kwasasa katika kikosi cha 837 KJ cha Chita mkoani Morogoro wameongeza kilimo cha mpunga kutoka ekari 1000 hadi 2500, huku kikosi cha Milundikwa kilimo cha mahindi kimeongezeka kutoka ekari 1000 hadi 1500.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa JKT, Kanali Hassan Mabena amesema kabla ya Mkuu huyo kuteuliwa kilimo, ufugaji na uvuvi ulikuwa ukifanyika kwa kiwango kidogo na mkakati waliokuja nao ni kuongeza uzalishaji na zana za kutosha.

“Aliniteua mimi kuwa Mwenyekiti wa kamati ambayo ina wajumbe wengine kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI), kamati ilikaa na kuandaa andiko ambalo lilitoa mwelekeo na kulikuwa na awamu mbili ya dharura na ya kimkakati,”amesema.

Ameeleza kutokana na kilimo cha awali kutegemea nguvu kazi ya watu na kuja na mkakati wa kuwa na zana za kutosha ambapo kwa kipindi cha mwaka mmoja yalinunuliwa matrekta 16 pamoja na zana mbalimbali na imesaidia kumudu kulima mashamba makubwa.

“Pia tulipima afya ya udongo kwenye mashamba yote ya kimkakati na kujua virutubisho vinavyotakiwa na tumefanya mapema kabla ya kuanza msimu wa kilimo, pia tuliwapa lengo makamanda wa kikosi kuhakikisha mashamba yote yanapimwa kwa kutumia GPS na wataalam,”amesema.

Hata hivyo, amesema kutokana na uzalishaji mkubwa kwenye masuala ya kilimo, Wizara ya Kilimo imeahidi kuwajengea maghala ili kuhifadhi mazao yao.

Kuhusu mifugo na uvuvi, amesema mikakati ni kuwa na ng’ombe wengi wa maziwa na kuangalia soko la nje na pia JKT ni eneo linalotumika wanafunzi kujifunza kwa vitendo kwenye sekta hizo.

Naye, Kamanda wa Kikosi 847 KJ cha Milundikwa JKT, Luteni Kanali Philemon Mahenge, amesema katika msimu wa 2020/21 walipewa lengo la kulima ekari 1500 na wamefanikiwa kulitekeleza na kwamba kwenye msimu ujao wanatarajia kulima ekari 2000.

Amebainisha wamekuwa wakitumia vijana wa kujitolea katika jeshi hilo na kupitia kilimo hicho wananufaika kupata mbinu bora za kilimo ambazo zitawasaidia watakapomaliza mikataba yao.