Home Mchanganyiko MWINGINE AKAMATWA IRINGA KWA KUZUSHA KUUMWA WA MH. MAGUFULI

MWINGINE AKAMATWA IRINGA KWA KUZUSHA KUUMWA WA MH. MAGUFULI

0

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA IRINGA, (ACP) RIENADA MILLANZI AKIONGEA NA WAAANDISHI WA HABARI AMBAO HAWAPO PICHANI. (PICHA NA DATUS MAHENDEKA, JESHI LA POLISI).
**********************************************

NA Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi

SIKU MOJA BAADA YA SERIKALI KUKEMEA NA KUTOA ONYO KWA WANAOZUSHA TAARIFA ZA KUUMWA MH. RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA JOHN MAGUFULI, JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA LINAMSHILIKIA TITO S/O AUGUSTINO KILIWA, MKULIMA MWENYE UMRI WA MIAKA 26, MHEHE, MKAZI WA KIJIJI CHA KIBENGU KILICHOPO WILAYA YA MUFINDI NA MKOA WA IRINGA KWA KUCHAPISHA KWENYE MTANDAO WA KIJAMII WA FACEBOOK TAARIFA ZA UZUSHI WA KUUMWA MH. RAIS.

AKIZUNGUMZA NA WAAANDISHI WA HABARI, KAIMU KAMANDA WA MKOA HUO, KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI, RIENADA MILLANZI, AMESEMA TAREHE 11/03/2021 KUPITIA UKURASA WA AKAUNTI YAKE YA FB MTUHUMIWA ALIANDIKA “RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANAUMWA” UJUMBE AMBAO ULILETA TAHARUKI NA MIHEMKO NDANI YA JAMII.

AMESEMA MTUHUMIWA HUYO AMEKAMATWA TAREHE 13/03/2021 SAA 13:00 HRS MCHANA KATIKA KIJIJI CHA KIBENGU KUPITIA KIKOSI MAALUM CHA POLISI KINACHOSHUGHULIKA NA MAKOSA YA MTANDAO.