Home Uncategorized MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WAFUNGWA GEREZA...

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WAFUNGWA GEREZA LA BUKOBA MANISPAA

0


KATIBU
Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Mansoor akikabidhi msaada wa taulo za kike
kwa ajili ya wafungwa wa Gereza la Bukoba Manispaa zilizotolewa na
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira kwa  matumizi
ya mwaka mzima
TIMU
ya Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira
na Uongozi wa UWT Mkoa na Uongozi wa UWT wilaya ya Bukoba Manispaa mjini
kabla ya kutoa msaada kwa wanawake Gezerani Bukoba leo

 
  BOX lilokuwa na Taulo za Kike za Kutosha za miezi sita za wanawake 53 waliopo Gezera la Bukoba
 
MBUNGE
wa Viti Maalumu (CCM) kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema
Lugangira leo ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanawake 53 ambao ni wafungwa waliopo
kwenye Gereza la Bukoba lilipo Manispaa  ambazo watazitumia kwa kipindi
cha miezi sita
 
 
Katika
tukio hilo la Makabidhiano ya taulo hizo Mh Mbunge Neema ambaye yupo
Dodoma kwa majukumu ya Kibunge, msaada huo ulikabidhiwa na leo na timu
ya Ofisi ya Mbunge ikiongozwa na Katibu Wake Kitaifa Judith, Katibu
Msaidizi Kagera Mansoor na Mratibu wa Ofisi Datius. Aidha, Chama Cha
Mapinduzi kupitia Umoja Wanawake Tanzania kiliwakilishwa na Paulina
ambae ni Katibu wa UWT Kagera, Sharifa ambae ni Katibu wa UWT Bukoba
Mjini na PS wa Ofisi ya UWT Mkoa. 
 
 
 
Katika
salamu zake Mh Mbunge Neema aliwatakia heri wanawake wote kote nchini
kwa kuazimisha siku ya wanawake duniani huku akihaidi kwamba atakikisha
mtoto wa kike hakosi shule kwa sababu ya kukosa taulo za kike na kwamba
ushiriki wake katika ziara ya Kamati ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Madawa ya
Kulevya ulimpa fursa ya kufika kwenye Gereza 2 (Njombe na Mbeya) hivyo
kumfanya atambue uhitaji wa taulo za kike pia kwa wanawake walio
gerezani na ndio maana akaamua kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa
mtindo huu.  
 
 
Mbunge
Neema  aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari
ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo
alisema suala la hedhi salama ni moja ya vipaumbele vyake hivyo
ataendelea kutafta mbinu mbalimbali za kupunguza changamoto hiyo.
 
 
Aidha
pia Mbunge Neema aliwasihi wanawake wajitambue na kujithamini ikiwemo
kufanya kazi kufa na kupona yaani kwa bidii kubwa sana ili waweza kupata
maendeleo
 
 
 
Akizungumzia
mambo ambayo anakusudia kuyafanyia kazi Mbunge Neema alisema mambo
ambayo atakwenda kuyafanyia kazi ni kupaza sauti na vipaumbele vyake
vikubwa kwenye maeneo ambayo hayatiliwi mkazo kutokana na  kuona kwa
sasa  ni wanawake wengi wanatesaka kwa kuachwa na mzigo mkubwa wa kulea
watoto peke yao.
 
Alisema
pili ni wanawake wengi wanafanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi lakini
pia ni wafanyabiashara wadogo na wakienda kwenye mabenki kutafuta mikopo
hawapati.
 
Alisema
jambo hilo limekuwa likiwapa vikwazo vikubwa sana kwao kufikia
maendeleo kutokana na kwamba wanapewa sheria kedekede ambazo hawaziwezi
na moja ya kujukumu lake ni kutathmini wafanye nini ili wanawake walio
kwenye sekta isiyorasmi waweze kuingia kwenye sekta iliyorasmi na waweze
kupata mikopo ambayo itawasaidia kuwainua kiuchumi.