Home Michezo WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT DAMAS NDUMBARO APANIA KUTUMIA MICHEZO KUKUZA...

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT DAMAS NDUMBARO APANIA KUTUMIA MICHEZO KUKUZA UTALII NCHINI

0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akibadilisha fimbo kutoka kwa Freddy Lukala ili kuweza kuupiga mpira kwenye muelekeo unaofaa wakati akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki  katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa ameshika fimbo kuupiga mpira wakati akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki  katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa  ameupiga mpira wakati akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki  katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na mchezaji mwenzake  Dkt. Aloyce Subhamilia  na mara baada ya  kufanya mazoezi mwishoni mwa wiki  katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo.
***************************
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema Wizara yake imeanza juhudi za kufungamanisha michezo na Utalii kwa maana ya Utalii wa Michezo ikiwemo ya Soka na Gofu
Amebainisha hayo  mwishoni mwa wiki wakati akifanya mazoezi ya gofu katik Uwanja  Gymkhana Gofu Klabu uliopo mkoani Morogoro aliyoyafanya kwa muda wa siku nne  asubuhi na jiono  kwa lengo la kukuza utalii kupitia mchezo wa Gofu.
Hatua hiyo ya uhamasishaji ya kufanya mazoezi ya Gofu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amefanya  wakati wa akifanya mikutano na Wadau wa Utalii iliyofanyika kwa muda wa siku nne mfululizo mkoani hapo.
Amesema Wizara imejipanga kuhakikisha inaufanya mchezo wa Gofu  kuwa kichochea cha kukuza  utalii kwa kuandaa mashindano yatakayo wakutanisha watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

  
Akizungumzia mikakati ya kukuza utalii wa michezo, Waziri Ndumbaro amesema ameiagiza Menejimenti ya Hifadhi ya Mikumi kuukarabati uwanja wa mpira wa miguu uliopo katikati ya Hifadhi hiyo ili timu mbalimbali ziweze kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mechi pamoja na kufanyia mazoezi ikiwemo timu ya Simba na Yanga.
Amesema kuukarabatiwa kwa uwanja huo kutasaidia kuongeza idadi ya Watalii wanaotembelea Hifadhi hiyo ambapo amesema  watu mbalimbali wakiwemo wachezaji na Mashabiki watakwenda  kuangalia mechi wakat huo huo watapata fursa ya  kuangalia makundi mbalimbali ya Wanyamapori wakiwa mbali kidogo ya  uwanja wakiwemo nyati, simba pamoja twiga 
Amesema katika nyakati za jioni Wanyamapori hao  hupendelea kula chakula karibu na Uwanja  huo, hivyo watazamaji wataweza kuufaidia 
Amesema mbali na uwepo wa uwanja wa mpira wa  miguu katika Hifadhi hiyo kuagiza ukarabatiwe, Pia ameagiza litafutwe eneo lingine  katika Hifadhi kwa ajili ya kutengeneza uwanja wa kikapu hatua itayosaidia kuwavuta Mashabiki na Wachezaji wa mpira wa miguu kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Pia, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali inatarajia kufanya mashindano makubwa katika uwanja wa Gofu wa TPC Moshi kwa yatakayowakutanisha Wachezaji wakubwa wa mchezo huo wa kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuitangazia Dunia kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na ni sehemu pekee utakayoweza kuupanda Mlima huu na sio kwingineko.
Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameipongeza  Klabu ya Simba kwa uamuzi wa kuwa Wazalendo kwa  kuitumia nembo ya “Visit Tanzania” katika  kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.