Home Mchanganyiko WAZIRI CHAMURIHO AMTAKA MKANDARASI BARABARA YA KASULU HADI MANYOVU KUBADILI MPANGO KAZI

WAZIRI CHAMURIHO AMTAKA MKANDARASI BARABARA YA KASULU HADI MANYOVU KUBADILI MPANGO KAZI

0

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza na Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Manyovu hadi Kasulu mkoani Kigoma, Kilomita 68.25. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Ujenzi) Architect Elius Mwakalinga, na Kulia kwake ni Wahandisi Washauri Juma Msonge pamoja na  Gelawdiwos.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akitoa maelekezo kwa Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa barabara ya Manyovu hadi Kasulu mkoani Kigoma Kilomita 68.25. Kushoto kwa Waziri ni Mhandisi Juma Msonge, Neymar HE na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Ujenzi) Architect Elius Mwakalinga.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Ujenzi) Architect Elius Mwakalinga akisaini kitabu cha Wageni katika maabara ya Kampuni ya Zhejiang Communications Construction Company Limited (ZCCC) inayojenga barabara ya Manyovu hadi Kasulu mkoani Kigoma Kilomita 68.25 kwa kiwango cha lami.

Mhandisi Juma  Msonge kutoka kampuni ya Beza Consulting Engineers akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho (wa kwanza kushoto) alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Manyovu hadi Kasulu mkoani kigoma, kulia kwa Waziri ni Architect Elius Mwakalinga Katibu Mkuu Wizara ya na Uchukuzi (sekta ya Ujenzi)

******************************************

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Manyovu hadi Kasulu mkoni Kigoma inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi Zhejiang Communications Construction Company Limited (ZCCC).

Akiongea na waandishi wa habari katika eneo la Buhigwe Waziri Chamuriho amemtaka Mkandarasi ZCCC anaejenga barabara hiyo  kutengeneza mpango kazi mpya utakaopelekea ujenzi wa barabara ya Manyovu hadi Kasulu kukamilika ndani ya muda na hivyo kuleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wanachi wa Mkoa wa Kigoma.

“Hakikisheni ujenzi wa majengo kwa ajili ya ofisi na makazi ya Mhandisi Mshauri wa mradi huu yanakamilika kwa wakati, ili ujenzi wa barabara hii uende kwa kasi sambamba na makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wake, mko nyuma ya muda mnapaswa kujipanga upya”

Kwa upande wake Eng. Haruna Maulid kutoka kampuni ya ZCCC inayojenga barabara hiyo alimueleza Waziri Chamuriho kuwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Manyovu Kasulu mpaka sasa una jumla ya watumishi 106 kati ya hao watumishi 20 wataalamu kutoka china na waliobaki ni wataalamu wa hapa nchini.

Nae Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis Choma, amewaambia waandishi wa habari kuwa  kipande cha barabara ya Manyovu hadi Kasulu kinachojengwa kwa kiwango cha lami, kina urefu wa Kilomita 68.25 na ujenzi wake unagharimu shilingi Bilioni 76.1 kwa mkataba wa miezi 36, ambao unatarajiwa kukamilika Tarehe 31/8/2023

Waziri Chamuriho aliongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Architect Elius Mwakalinga pamoja na Mkurugenzi wa Barabara  Mhandisi Rogatus Mativila