Home Michezo YANGA YAZIDI KUPOTEA MBIO ZA UBINGWA,YACHAPWA 2-1 NA COASTAL UNION

YANGA YAZIDI KUPOTEA MBIO ZA UBINGWA,YACHAPWA 2-1 NA COASTAL UNION

0

……………………………………………………………………………..

Klabu ya Yanga imepokea kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake tukishuhudia Yanga kukosa penati ambayo ilipigwa na Tuisila Kisinda lakini goli kipa wa Coastal Union kuonesha makali yake kwa kudaka penati hiyo.

Coastal Union walianza kupata bao mnamo dakika ya 10 kupitia kwa nyota wao Francis Msagati na kuwafanya kuongoza kabla ya Tuisla Kisinda kusawazisha bao mnamo dakika ya 37 ya mchezo.

Katika kipindi cha pili Yanga ilionesha kuhitaji kuongeza bao ili kuondoka na ushindi lakini juhudi zao ziligonga mwamba hivyo Coastal Union wakatumia madhaifu madogo ya mabeki wa Yanga na kupata nafasi kupitia kwa Mshambuliaji wao Mudathir Abdallah dakika ya 84 ya mchezo na kuondoka na Ushindi.