Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Selemani Jafo,akisikiliza taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa Barabara za Mijini na Vijijini kutoka TARURA Mhandisi Mohammed Mkwata mara baada ya Waziri kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali huku akionyeshwa kutoridhishwa na kazi ya ujenzi huo Leo March 3,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akimtaka mkandarasi kuacha visingizio na kukamilisha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali kwa wakati mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo March 3,2021 jijini Dodoma.
Muonekano wa barabara ya kuingia Hospitali ya Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya Chamwino.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akitoa maelezo kwa Meneja wa TARURA kutoka halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Mhandisi Nelson Maganga mara baada ya kukagua mradi wa barabara ya kuingia Hospitali ya Uhuru katika Wilaya Chamwino huku akimtaka Mkandarasi kukamilisha Machi 14 mwaka huu katika ziara yake ya kikazi leo March 3,2021.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukagua mradi wa barabara ya kuingia Hospitali ya Uhuru katika Wilaya Chamwino leo March 3,2021.
………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,amesema kuwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara za mji wa serikali Mtumba.
Kauli hiyo ameitoa leo March 3,2021 jijini Dodoma baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo huku akimuagiza Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kwa matakwa ya mkataba wake Julai 30, mwaka huu.
Mhe. Jafo ameitaka TARURA kuhakikisha kuwa ujenzi wa barabara hizo za mji wa serikali unakamilika Julai 30, mwaka huu na kuwa kama kikwazo ni kukosekana kwa saruji hiyo nyepesi basi waangalie uwezekano wa kutumia saruji yenye mgandamizo wa juu.
“Sijaridhishwa na kasi hii maana ipo chini kwa asilimia sita kwa maana hiyo sihitaji mjadala wa aina yoyote nataka ifikapo Julai 30 mradi huu uwe umekamilika, haiwezekani uchelewe kwa kigezo cha kukosekana Saruji aina ya 32.5N hivyo angalieni namna ya kutafuta suluhisho ya hili,” amesema Jafo.
Waziri Jafo amewataka TARURA waifanyie utafiti wa kimaabara saruji aina ya 42.5N ambayo kwa sasa inapatikana madukani ili kuona kama inafaa kutumika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Awali, akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi, Mkurugenzi wa Barabara Mjini Mhandisi Mohammed Mkwata amesema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa Februari mwaka huu utekelezaji umefikia asilimia 63 na ilitakiwa kuwa asilimia 69 kwa mujibu wa mpango wa kazi wa mkandarasi.
“Katika kipindi hicho mkandarasi hakuweza kupata saruji aina zote za 32.5N na 42.5N kwa kadiri ya mahitaji halisi hali ambayo iliathiri kazi za ujenzi wa vivuko na ujenzi wa tabaka la kwanza la barabara ambalo nalo linahitaji saruji,” amesema Mhandisi Mkwata
Aidha amesema kuwa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini(TARURA) kupitia Mhandisi mshauri itaendelea kusimamia mradi huu kwa karibu zaidi ikiwa ni pamoja na mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuona kuwa mradi unakamilika kwa muda uliopangwa.
Katika hatua nyingine,Waziri Jafo ametembelea mradi wa barabara ya kuingia Hospitali ya Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya Chamwino huku akiridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo na kuahidi kuwa ifikapo Machi 15 atafika eneo hilo tena kuona ujenzi ulivyokamilika.
Waziri Jafo, amefanya ziara katika miradi hiyo miwili, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara zake za kikazi kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo na kutolea maelekezo kwa watendaji wa serikali katika Jiji la Dodoma