Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge ,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri wilayani Chamwino kusikiliza Malalamiko ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji hicho wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kumuuzia muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga,akizungumza kwenye Mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri wilayani Chamwino ambao wanadai ardhi yao kuuzwa kwa Muwekezaji na Halmashauri ya Wilaya hiyo leo March 3,2021.
Mbunge wa jimbo la Chamwino Mhe. Deogratus Ndejembi ,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri wilayani Chamwino wanalio katika mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji hicho wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kumuuzia muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Maduka Kessy,akipokea maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge ambaye amemtaka kuunda kamati maalumu itakayokwenda kuchunguza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kumuuzia muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Mwegamile Kata ya Buigiri wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge (hayupo pichani) wakati alipofika kusikiliza malalamiko yao ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji hicho wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kumuuzia Muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mgogoro Bw.Gabriel Masinga akisoma taarifa ya wananchi wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri wilayani Chamwino wanaolalamikia mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji hicho wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Kumuuzia Muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Mkulima wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri wilayani Chamwino Bw.Amos Mtagomwa akiiomba Serikali kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji hicho wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Kumuuzia Muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwegamile akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge kwa kufika katika kijiji hicho kusikiliza Malalamiko ya wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji hicho wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kumuuzia Muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Mkuu wa Idara ya Kilimo halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Godfrey Mnyamale,akisoma taarifa fupi ya Shamba la Zabibu la Chinangali II ambalo lipo katika Mgogoro wa ardhi Kati ya wananchi wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri wilayani Chamwino wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa Kumuuzia Muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Maduka Kessy kuunda kamati maalumu itakayokwenda kuchunguza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji cha Mwagamile kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kumuuzia Muwekezaji eneo wanalodai ni lao leo March 3,2021.
……………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Chamwino
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Maduka Kessy kuunda kamati maalumu itakayokwenda kuchunguza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kijiji cha Mwegamile kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wanaoituhumu Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kumuuzia muwekezaji eneo wanalodai ni lao.
Akizungumza leo March 3,2021 alipofika katika Kijiji hicho kwa lengo la kusikiliza pande zote mbili Dkt Mahenge amesema ni lazima iundwe tume huru itakayoweza kuchunguza kwa undani mgogoro huo ili ijulikane mwenye uhalali na eneo hilo ni wananchi au halmashauri hiyo.
“Natoa siku 14 wiki mbili kamati hiyo ije na majibu ya uchunguzi ni nani mwenye haki na hili eneo kamati ichunguze ukubwa wa eneo na uhalali wake, matumizi yaliyopo kwa sasa na baadaye, na ijiridhishe madhara yanayoweza kutokea endapo eneo hilo litamegwa” amesema Dkt Mahenge.
Amesema baada ya kusikiliza pande zote mbili amebaini kuwa eneo hilo ni mali ya Halmashauri tangu mwaka 1984 baada ya wawekezaji waliopewa eneo hilo kushindwa kuliendeleza ndio wananchi wakaendelea kulimiliki vizazi na vizazi mpaka sasa mgogoro unaibuka halmashauri inapotaka kuuza hilo eneo kwa muwekezaji wakati wananchi wamekaa katika eneo hilo kwa mda mrefu.
Hivyo ameitaka kamati hiyo itakayoundwa kuchunguza vielelezo vyote vinavyohusu eneo hilo tangu wawekezaji wa awali hadi sasa na ametaka kamati hiyo ijumuishe wananchi, TAKUKURU, watu kutoka halmashauri na wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Aidha ameagiza muwekezaji huyo kusitisha shughuli zote hadi hapo kamati itakapokuja na majibu ya uhalali wa eneo hilo ndipo shughuli nyingine ziendelee kama kawaida baada ya kujulikana hilo eneo ni mali ya nani.
Awali wananchi kupitia kwa mwakilishi wao Bw. Gabrial Masinga walimwambia Mkuu wa Mkoa kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu ambapo Halmashauri iliwashtukiza kuwa wana shamba ekari 350 na wanahitaji shamba hilo kwa ajili ya kilimo cha zabibu wanasema ulitokea msuguano lakini mwisho wa siku wananchi waliahidiwa fidia na kwamba wataingizwa katika mradi huo bure.
Wanasema lakini mpaka sasa hakuna mwananchi aliyelipwa fidia au kufikiliwa kupewa eneo la kulima na kuchunga mifugo hali inayosababisha kilio kikubwa kwa wananchi kwa kupoteza mashamba kwa ajili ya mradi wa kilimo cha zabibu.
Ameongeza kuwa “ Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwenye mgogoro huu wapo wazee, watu wazima, yatima, wajane na walemavu ambao wanalia usiku na mchana kwa kadhia hii tunakupatia orodha ya wananchi walioathirika na uporwaji wa ardhi ujionee mwenyewe kuwa kuna lundo kubwa la watu walioathirika na zoezi hili” amesema Masinga.
Wamesema mnamo januari 23, 2021 waligundua kuwa halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeuza eneo lao lenye ekari 400 kwa kampuni ya Mega Beverages Limited ambapo kwenye kikao afisa kilimo aliutaarifu umma kuwa halmashauri ya Wilaya inamiliki ekari 1622 huku wakidai huo ni uporaji wa ardhi yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kilimo halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Godfrey Mchamale, akitoa maelezo ya Halmashauri amesema awali shamba hilo kupitia vikao halali waliliuza kwa muwekezaji mmoja 1984 na kushindwa kuliendeleza ndio likarudi kwenye umiliki wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Na baada ya kurudi kwenye umiliki wa Halmashauri likaendelea kutumiwa na wananchi na walipotaka kuliuza kwa muwekezaji wananchi wakadai eneo hilo ni mali yao halali, mwaka 2020 halmashauri ilipitia njia zote za kuomba ekari 400 kwa ajili ya muwekezaji na wananchi walikubali kwa sharti la muwekezaji huyo kushiriki katika shughuli za kijamii na wakakubaliana ajenge shule.
Nae Mbunge wa jimbo la Chamwino Mhe. Deogratus Ndejembi amesema wananchi hao hawapingi kujengwa kwa kiwanda hicho kwani pia faida kwao kwa kupata ajira bali kulikuwa na sintofahamu baada ya kuona muwekezaji ameanza baadhi ya maandalizi huku wao wakiwa hawajui lolote katika eneo hilo.