Home Michezo MBIO ZA AYAC ZITAKAZOSHIRIKISHA WATOTO KUFANYIKA MACHI 28 MWAKA HUU.

MBIO ZA AYAC ZITAKAZOSHIRIKISHA WATOTO KUFANYIKA MACHI 28 MWAKA HUU.

0

******************************************
NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.
Mashindano ya mbio za  Arusha youth athletics championship{AYAC} yanayohusisha watoto wa miaka 6 hadi 14 kufanyanyika machi 28,2021 kwa lengo la kuongeza ushiriki wa watoto katika michezo pamoja na kukuza kizazi ambacho kitakuwa na uwelewa wa taaluma katika riadha.
Akizungumza  na waandishi wa habari mkoani Arusha muandaaji wa mashindano ya AYAC Juliana Mwamsavua alisema  wamefungua dirisha la usajili wa mbio hizo ambazo zitashirikisha watoto wa shule za msingi na sekondari ambao zitawahusisha watoto 302 kutoka shele mbalimbali za jiji la Arusha.
Alisema mashindano hayo ambayo wameandaa kwa kushirikiana na chama cha riadha wilaya ya Arusha, mkoa na taifa ambayo yatakuwa na mbio mbalimbali ikiwemo mbio ndefu, za kati, fupi za vijiti na viunzi ambayo yatafanyika katika uwanja wa Sheik Amri Abeid Kaluta uliopo mkoani hapa. 
“Tumetoa mwaliko kwa shule mbalimbali ila tunaomba watoe udhibitisho mapema kwani wale watakowahi t undo wataweza kushiriki na tumeshaweka idadi maalum kuwa watakaoshiriki ni watoto 302 tu,”alisema Juliana.
Alifafanua kuwa watoto watakao shinda katika mashindano hayo AYAC watakuwa wanadhaminiwa kwenda katika mashindaya Afrika mashari, Afrika na kimataifa hivyo wazazi wawape watoto nafasi ya kushiriki fursa zilizopo katika mashindano hayo kwani kupitia michezo wanaweza kutoka kimaisha.
“wapeni nafasi watoto waje washiriki katika mashindano kwani riadha inachangia katika pato la taifa na hamjui baade motto anaweza kuwa kuwa nani, tumefungua usajili kwanzia sasa na mnaweza kutupata kupitia namba za simu 0754 623517,” Alieleza Juliana. 
Kwa upande wake makamu wa rais wa chama cha riadha Tanzania,John Bayo alisema mbio za uwanjani zilikuwa hazijapewa kimpaumbele hivyo anamshukuru mwandaaji wa mbio hizo kwa kuwekeza kwa watoto ambao ndio wanariadha wa kesho japo baadhi ya shule wanafanya kwa kiasi kidogo.
“Mbio hizi za watoto nia msingi wa riadha kwani umri huu mdogo ni umri mzuri ambao utakuza taaluma ya riadha lakini pia unakuza vipaji na baadae kuja kuwa na wariadha wazuri zaidi hivyo niwaobe waandaji pia kaika mashindano mengine mmuweze kushirikisha wilaya nyingine ili kwa pamoja tuweze kunufaika na fursa hii,” alisema Bayo.
Rogath Stehen katibu mkuu wa chama riadha mkoa wa Arusha  alisema kuwa  mbio moja ni muhimu sana kwani zinalenga watoto wadogo ambazo zitakuwa na mbio nyingi za watoto ili kuhakikisha wanaendeleza vipaji vya watoto ili kuwa na mnyororo wa wanariadha ambao wakistaafu wakubwa na wao wanaendeleza.
“Hatuwezi kwenda kwenye viwango vya kimataifa kama huku chini kwenye mizizi hatujapajenga vizuri na tunatamani katika olimpiki ya mwaka 2024 tuwe na idadi kubwa ya wawakilishi lakini kama hatutajijenga vizuri hatutaweza kufanikiwa hivyo wazazi na walimu muwasajili watoto wenu kwani mashindano haya yataendeshwa kitaalamu na usajili ni bure,” Alieleza.