Home Mchanganyiko GST YAPATA MAFUNZO JUU YA UTEKELEZAJI WA SHERIA, KANUNI, TARATIBU NA MIONGOZO...

GST YAPATA MAFUNZO JUU YA UTEKELEZAJI WA SHERIA, KANUNI, TARATIBU NA MIONGOZO YA UNUNUZI WA UMMA KUTOKA PPRA

0

…………………………………………………………………………………………

Na. Samwel Mtuwa- GST.

Leo Machi 2, 2021 Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania(GST) imeanza kupata mafunzo maalum ya siku 4 kutoka Mamlaka ya Kudhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) juu ya uzingativu katika Sheria,Kanuni,Taratibu na Miongozo ya Ununuzi wa Umma.

Akiongea wakati wa kuwakaribisha Wawezeshaji kutoka PPRA, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba alisema kuwa utendaji mzuri katika Utumishi wa Umma ni kufuata Sheria na kuheshimu taaluma husika.

Kwa upande wake muwezeshaji kutoka PPRA Ndugu Frank Yesaya akiongea wakati wa kuanza mafunzo hayo alisema kuwa lengo la mafunzo haya ni kuijengea uwezo GST juu ya matakwa ya Sheria na Kanuni za Ununuzi wa Umma katika kufanya Ununuzi wa bidhaa pamoja na kupata huduma.

Akifafanua wakati wa mafunzo hayo , muwezeshaji mafunzo alifafanua kuwa kwa kuzingatia kifungu Cha 9 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma , PPRA imepewa jukumu la kujenga uwezo kwa Taasisi Nunuzi za Umma ili ziweze kufuata sheria ,Kanuni,Taratibu na miongozo husika ya Ununuzi ili kuleta tija na nidhamu katika matumizi ya fedha za Umma.

Katika mafunzo haya ya siku 4 mada mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na Sheria , Kanuni na Marekebisho yake ya Ununuzi wa Umma , Njia na aina mbalimbali za ununuzi na usimamizi wa Mikataba , mada juu ya mifumo ya michakato ya Zabuni.