Wakuu waWilaya zaMkoawaSingida(kwenye mstari wa kwanza) |
AfisaUhamasishaji Uwekezaji Mkuu kutoka Kituo cha
Uwekezaji nchini, Joyce Shundu akiwasilisha mada ya“Mazingira na Fursa za Uwekezaji Nchini”amepongeza jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na MkoawaSingida
1. |
.
Viongozi
wa Wachimbaji Madini Mkoa wa Singida wakiwa kwenye banda lao
wakionyesha madini mbalimbali kwa wadau waliotembelea banda la wachimbaji wa madini Mkoa wa Singida (SIREMA).
Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakionyesha bidhaa zao
- RAS ASEMA MKOA UMEJIANDAA KIKAMILIFU
Na John Mapepele, Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe,
Dkt. Rehema Nchimbi amewataka Wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuwekeza
kwenye Mkoa wa Singida kwa
kuwa Mkoa huo umebarikiwa kuwa na fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo bado
hazijatumika kikamilifu.
Akifungua Kongamano la Mwongozo
wa Uwekezaji kwenye Mkoa wa Singida
kabla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo huo, Dkt. Nchimbi amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo
endapo fursa zake zikitumika
utachangia katika maendeleo ya Mkoa na
nchi kwa ujumla
Amezitaja baadhi ya fursa
zilizopo kwenye Mkoa wa Singida kuwa
ni pamoja na nishati ya mafuta asilia na
gesi, madini, kilimo cha alizeti, korosho,utalii,
ufugaji wa nyuki na kuku pia uwekezaji
kwenye sekta ya michezo ambapo amesema ni zamu ya Mkoa wa Singida kuchangia
kikamilifu kwenye uchumi wa nchi.
Akitoa mada kuhusu Uwekezaji wa Alizeti mkoani Singida,
Mratibu wa Utafiti wa Alizeti nchini, Frank Reuben amesema zao la alizeti ndiyo zao pekee
linaloweza kuuvusha mkoa wa Singida
kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa
mkoa wa Singida ndiyo unaongoza
hapa nchini kwa kulima zao hilo.
Ametaja baadhi ya maeneo ya fursa za uwekezaji kwenye kilimo cha
Alizeti kuwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji wa mbegu, Kilimo bora
(mesto) cha alizeti na ufugaji nyuki (Agro-apiculture) na uendelezaji wa
viwanda vya kuchakata alizeti, chakula cha mifugo na mazao ya nyuki
Mtafiti wa zao la Korosho, kutoka
Taasisi ya Utafiti wa mazao ya Kilimo (TARI) Dkt. Fortunatus Kapinga akitoa mada ya zao la Korosho nchini
amesema Mkoa wa Singida una ardhi nzuri
yenye rutuba ambayo inafaa sana kwa zao la korosho ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini hivyo ni fursa pekee kwa wawekezaji kuja kufanya uwekezaji katika mkoa huu.
Amezitaja baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye zao la
Korosho kuwa ni pamoja na juisi, jamu,mvinyo, maziwa na siagi ambapo amesema
kauli mbiu ya mkoa kwenye uwekezaji kwamba
“ni zamu yetu” ikitafsiriwa kwa vitendo italeta mageuzi makubwa katika mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wanawake wachimbaji
Madini Mkoa wa Singida, Martha Kayaga
amepongeza Serikali ya awamu ya Tano inayoongizwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa
jitihada kubwa inayofanya kuwashilikisha wachimbaji wazawa kwenye sekta ambapo
ameiomba Serikali kuangalia namna bora ambayo itawawezesha wajimbaji wadogo
wadogo kupata mitaji hususan vifaa ili waweze kuongeza tija katika sekta hiyo.
Pia Bi. Kayaga ameiomba
Serikali kuwaangalia wachimbaji wanawake
kwa jicho la pekee kwa kuwa wao ni nguzo muhimu kwenye familia na kwamba
asilimia 10 inayotengwa kwenye Halmashauri imekuwa ikielekezwa kwenye sekta nyingine
ambapo amesisitiza endapo itaelekezwa kwa akina mama wachimbaji wadogowadogo
itasaidia kuinua hali za uchumi kuanzia kwenye ngazi ya kaya na Taifa kwa
ujumla.
Kwa upande wake, Afisa Uhamasishaji Uwekezaji Mkuu kutoka
Kituo cha Uwekezaji nchini, Joyce Shundu
akiwasilisha mada ya “Mazingira
na Fursa za Uwekezaji Nchini” amepongeza
jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na Mkoa wa Singida kwa
kwenye uwekezaji na kutoa wito kwa
wawekezaji kuwahi kuwekeza kwenye fursa
za kipekee zinazopatikana mkoani hapa.
Awali katika salamu za
utambulisho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka
Watendaji wote wa Serikali Mkoa wa Singida kuhakikisha wanajituma kufanya kazi
kwa weledi kwenye utoaji huduma bora kwa
wawekezaji ili azma ya Serikali ya kutaka uwekezaji wenye tija itimie na
maisha bora kwa watanzania ifikiwe.
Dkt. Lutambi amesema Serikali ya
Mkoa imeshaandaa mazingira wezeshi kwa
wadau na wawekezaji makini kuja kuwekeza
kwa kuzingatia sheria na taratibu
za nchi.