Home Michezo NAMUNGO YATINGA HATUA YA MAKUNDI CAF,YACHAPWA 3-1 NA PRIMEIRO DE AGOSTO YA...

NAMUNGO YATINGA HATUA YA MAKUNDI CAF,YACHAPWA 3-1 NA PRIMEIRO DE AGOSTO YA ANGOLA

0
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna
Licha ya kupoteza kwa mabao 3-1 kutoka kwa Primeiro De Agosto ya  Angola,Timu ya Namungo imetinga  hatua ya  makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) kwa jumla ya magoli 7-5 ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki Mashindano  ya Kimataifa tangu ipande Ligi Kuu Tanzania bara.
Mechi zote zimechezwa katika ardhi ya Tanzania katika uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam Chamazi Complex unaomilikia na timu ya Azam FC.
Mechi ya kwanza Namungo walishinda mabao 6-2 na Mchezo wa Leo Namungo wamekubali kufungwa mabao 3-1 na wageni Primeiro De Agosto kutoka Angola.
Kwa matokeo hayo Namungo wameangukia kundi D ambapo watakuwa pamoja na Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids FC ya Misri na Nkana FC ya Zambia.