Home Michezo TASWA FC KUSHIRIKI BONANZA LA MAKAMPUNI

TASWA FC KUSHIRIKI BONANZA LA MAKAMPUNI

0

………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa FC) inatarajiwa kushiriki mashindano ya makampuni.
Hiyo ni mara yaa pili kwa mashindano hayo kufanyika na mwaka jana ambaye bingwa mtetezi ni Dawasa ambao waliwafunga TRA walipokutana fainali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa mashindano hayo Peter Ngasa alisema kuwa mashindano yatafanyika kwenye viwanja vitatu vya JK Park, Gymkhana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ngasa alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Aprili 4, mwaka huu na tumu zilizothibitisha ushiriki huo ni Popaoa Timu nyingine zilizothibitisha kushiriki ni Silent Ocean, TICTS, Ecobank, Asas Rangers, Tanesco na Twiga Cement.
“Optimam Investment kama waandaaji wa mashindano haya ya makampuni, maandalizi yanakwenda vizuri.
” Tayari baadhi ya timu zimethibitisha ushiriki huo kati ya hizo ni mabingwa watetezi DAWASA,” alisema Ngasa.
Mwenyekiti wa Taswa, Majuto Omary kwa upande wake alisema kuwa “Wanashukuru kuwa sehemu ya timu shiriki katika mashindano hayo tumepanga kufanya vema.
” Kwani kwetu ni nafasi pekee ya ushiriki, kwani tulishawahi kushiriki mashindano ya aina hii mkoani Arusha na kuchukua makombe mara 18 tulizoshiriki,”alisema Omary.