Home Michezo NAMUNGO FC MGUU NDANI HATUA YA MAKUNDI CAF,YAICHAPA 6-2 DE AGOSTO YA...

NAMUNGO FC MGUU NDANI HATUA YA MAKUNDI CAF,YAICHAPA 6-2 DE AGOSTO YA ANGOLA

0

Na,Mwaandishi wetu,Dar es Salaam

Timu ya Namungo FC imejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) baada ya kupata ushindi wa mabao 6-2  dhidi ya wapinzani wao Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano.

Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa  Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam,ambapo Agosto walikuwa wenyeji baada ya CAF kuamua mechi zote zichezwa Tanzania.

Wenyeji walipata bao kwa njia ya Penalti dk.11 Moya na la pili limefungwa Dk.50 Salvador huku Mabao ya Namungo FC  yamefungwa na Hashim Manyanya dak.29, Sixtus Sabilo dk.37 na 60 aliyefunga mawili,Reliants Lusajo dk.55,Erick Kwizera dk.65 na Steven Sey dk.70.

Kwa ushindi huo Namungo wanasubiri Mchezo wa marudiano utakaochezwa uwanja huo huo wa Chamazi huku wakiwa wenyeji utakaopigwa Februari 25 mwaka huu.