Home Michezo MEYA MANISPAA AKABIDHI MILIONI 3 KWA LIPULI FC

MEYA MANISPAA AKABIDHI MILIONI 3 KWA LIPULI FC

0
Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akizungumza na wachezaji wa lipuli fc
baadhi ya wachezaji Lipuli fc
Meya akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Lipuli.
*****************************************
NA DENIS MLOWE IRINGA
MEYA wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada ametoa kiasi Cha sh. Milioni 3 kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa  timu ya soka ya Lipuli fc ukiwa ni morali kwao kuweza kufanya vyema katika mchezo wao dhidi ya Mawenzi Market.
Licha ya kuwakabidhi kiasi hicho, Meya wa Manispaa Ngwada aliweza kula chakula Cha pamoja na wachezaji hao na viongozi wao huku akiwataka kuhakikisha wanafanya vyema katika michezo iliyobaki ya ligi soka daraja la kwanza.
Katika kikao hicho pia walikuwepo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga ambaye alipata muda wa kututia moyo na kuwaasa vijana, Alikuwepo Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Iringa Mama Ritha Kabati ambaye pia alifurahi kukutana na timu na ameahidi kuisaidia zaidi na kushiriki kuhakikisha timu inapanda, alikuwepo Msaidizi wa mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu na alikuwepo Mwenyekiti wa Vijana Iringa Mjini(CCM)Salvatory Ngelela.
Viongozi wa Lipuli na Meya wamekubaliana kushirikiana kwa karibu zaidi ili timu ipande na Meya amefungua milango ya ofisi yake kwa kila mtu anayetaka kumuona kwa ajili ya kuisaidia Lipuli wakiwemo viongozi ambao wameruhusiwa kwenda kumuona wakati wowote.
Kwa upande wao ,Uongozi wa Lipuli unamshukuru sana na kama viongozi wameahidi kutoa ushirikiano na kuwa wawazi zaidi katika uendeshaji wa timu.
Aidha Viongozi hao wamewakumbusha wana Iringa na wapenzi na mashabiki wa Lipuli na kuwakaribisha kwenye Mechi ya leo ambayo Mstahiki Meya atakuwepo na ataongoza safu ya ushangiliaji.