Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar amefariki dunia.
Rais  wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi amesema Makamu huyo amefariki leo  saa 5:26 Asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.