Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wadau kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) walipofanya ziara ya mafunzo Wizarani.
Sehemu ya Wadau kutoka NDC wakifuatilia mhadhara uliokuwa ukitolewa na viongozi wa Wizara
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau na uongozi wa NDC na Watendaji wa Wizara.
Mkurugenzi wa Siasa,Ulinzi na Usalama Balozi Stephen P. Mbundi akifafanua jambo kwa wadau kutoka NDC wakati walipofanya ziara ya mafunzo Wizarani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akipokea kalenda kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha NDC Brigedia Jenerali Ibrahim Michael Muhona baada ya kumaliza kutoa mhadhara.
*************************************
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge amaeleza kuwa nguvu ya ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya kikanda na kimataifa bado upo imara, licha ya Tanzania kutoa mchango mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika na uanzishwaji wa Jumuiya za Kikanda kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hadi hivi sasa Tanzania bado ni kinara katika kutetea na kuadai maslahi ya Bara la Afrika.
Balozi Brigedia Jenerali Ibuge, amebainisha haya alipokuwa akizungumza na wadau kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) ambao waliitemebelea Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza kuhusu majukumu ya Wizara, hasa katika kutetea maslahi ya Nchi nje ya mipaka ya Tanzania. Katibu Mkuu aliendelea kubainisha kuwa Wizara katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje pamoja na mambo mengine inahakikisha kuwa inatoa kipaumbele kwenye kulinda maslahi ya Nchi ikiwewo ulinzi na usalama.
NDC kwa upande wao wameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanywa na Ofisi zake za Ubalozi sehemu mbalimbali duniani katika kutangaza fursa zilizopo nchini kwenye maeneo yao ya uwakilishi madhalani utalii, biashara ya madini na mazao ya kilimo, pia kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.