Home Mchanganyiko ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI MKOA WA...

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI MKOA WA DAR ES SALAAM

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemenja kuhusu ukamilishaji wa Mradi wa kisima kikubwa cha Maji Safi chenye urefu wa mita 600 kilipo eneo la Kigamboni wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku ya pili kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maji  na Mazingira katika Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 14,2021. kulia ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu alipokua akitembelea na kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Maji Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 14,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea na kukagua Utelelezaji wa Miradi ya Maji Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam  leo Febuari 14,2021. katikati ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu kushoto Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakari Kundenge na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Maji General Davis Mwamunyange.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya Temeke katika eneo la Kijichi Mbagala alipokua katika ziara yake ya siku ya pili kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 14,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajasiriamali wa Soko Jipya la Kijichi Mbagala Wilaya ya Temeke, wakati alipokua katika ziara yake ya siku ya pili kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 14,2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)