Home Michezo YANGA YAPUNGUZWA KASI MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU VODACOM

YANGA YAPUNGUZWA KASI MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU VODACOM

0

Na Mwandishi Wetu
VINARA, Yanga SC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Mbeya City   Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Yanga walipata bao dakika ya 84 likifungwa na Deus Kaseke hata hivyo Mbeya City walisawazisha bao dakika ya 90 +2 kwa njia ya Mpira ambao ulitokana beki Yassin Mustapha kuunawa na mshambuliaji Pastory Athanas akafunga mkwaju huo  uliompita kipa, Metacha Mnata.

 Kwa matokeo hayo Yanga bado wanaongoza Ligi kwa kufikisha Pointi 45 wakiwa wamecheza mechi 19 huku Mbeya City wakifikisha Pointi 15

Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; Haroun Mandanda, Kenneth Kunambi, Mpoki Mwakinyuki, David Mwasa, Babilas Chitembe, Edgar Mbembela, Pastory Athanas, Mathew Robert, Jean Didier/Abasarim Chidiebere dk88, Hamisi Thabit/Herbet Lukindo dk76 na Kato Yayo/Juma Shamvuni dk59. 
Yanga SC; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto,  Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong, Fiston Abdul Razak/Ditram Nchimbi dk74 na Farid Mussa/Deus Kaseke dk67.