Home Mchanganyiko TANESCO KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI KWA KUWAPELEKEA UMEME

TANESCO KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI KWA KUWAPELEKEA UMEME

0

Afisa Mahusiano wa TANESCO Samia Chande (kulia) akijadiliana jambo na Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Andrew Lucas (kushoto) muda mfupi kabla ya mahojiano ya waaandishi wa habari na Meneja huyo kwenye Banda lao katika Maonesho ya NEEC yanayoendelea Jijini Arusha.

Afisa Masoko wa TANESCO Adelina Lyakurwa (kushoto aliekaa) akiwa na mwenzake Richard Sekeyani (kulia) wakimuonyesha kitabu cha kutia saini mteja Naomi Chacha mara baada ya kumaliza kuhudumiwa alipofika kwenye banda la Shirika hilo kupata maelekezo na taarifa mbalimbali.

Afisa wa TANESCO Richard Sekeyani (aliekaa) akizungumza na mteja Naomi Chacha aliefika kwenye Banda la Shirika hilo kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali na huduma zitolewazo na TANESCO kwenye maonesho ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika kwa siku saba Jijini Arusha.

………………………………..

Na: Hughes Dugilo, ARUSHA.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga katika kuhakikisha linawawezesha wananchi kiuchumi kwa kupeleka umeme katika maeneo yote nchi nzima kwa lengo la kuboresha uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Mhandisi Andrew Lucas alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha na kusema kuwa Jiji la Arusha tayari wamesha sambaza umeme kwa asilimia 80.

“Kwa hapa Arusha Jiji umeme umefikia karibu asilimia 80 maeneo yote yana umeme maeneo yaliyobaki asilimia 20 tunapambana kumalizia na tunahakikisha katika kipindi hiki cha miaka mitano ya muheshimiwa Rais tutakamilisha yote wananchi watakuwa na umeme wa uwakika” Amesema mhandisi Andrew.

Amesema kuwa katika kuhakikisha TANESCO inawawezesha wananchi kiuchumi wanahakikisha wanapeleka umeme kwa wananchi kwa gharama nafuu lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yao ya msingi.

Aidha ametoa wito kwa watanzania kuwekeza kwenye Sekta ya viwanda na kwenye maeneo tofauti wanayoyahitaji kwani shirika lipo tayari kuwekeza kwenye maeneo yote wanayoyahitaji.

Mhandisi Andrew amewasihi wakazi wa Jiji la Arusha kufika kwenye banda lao katika maonesho hayo ili kuweza kujipatia huduma mbalimbali na kufahamu miradi ya TANESCO inayotekelezwa katika Mkoa wa Arusha na nchi kwa ujumla.

“kwa sasa hivi Arusha kwa bajeti hii tunayoendelea nayo ya 2021 tuna miradi midogo yenye thamani ya shilingi Bilioni 10 kwa Arusha ambayo sasa hivi tuna asilimia 80 ya kutekeleza miradi hiyo kwa hiyo tunaamini mpaka tufike mwezi wa nne tutakuwa tumeshakamilisha miradi yote hiyo” Ameongeza Mhandisi Andrew Lucas.