Home Michezo MASHABIKI WA YANGA WASHINDA MAMILIONI YA M-BET

MASHABIKI WA YANGA WASHINDA MAMILIONI YA M-BET

0

Meneja masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kulia) akiwakabidhi mfano wa hundi kwa Dominic Mdimi (wa kwanza kushoto) na Valentino Ngolle baada ya kufanikiwa kubashiriki kwa usahihi mechi 12 za  ligi mbalimbali duniani.  Washindi ambao pia ni mashabiki wa Yanga walishinda Sh85,996,360.

……………………………………………………………………………………………………….

Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam.

Mashabiki wawili wa mpira wa miguu wamejishindia  jumla ya Sh85,996, 360 baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya michezo 12 ya mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.

Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi aliwataja washindi hao kuwa ni Dominic Mdimi ambaye anashabikiwa klabu ya Yanga ambapo amefanikiwa kushinda kwa mara ya pili droo ya Perfect 12. Mdimi alishinda mwaka Oktoba 2019 na kushinda Sh 36 million.

Mushi alimtaja mshindi mwingine ni Valentino Ngole wa Njombe  ambaye ameshinda kwa mara ya kwanza katika kushinda droo hiyo. Ngolle pia ni shabiki wa Yanga.

Alisema kuwa Mdimi na Valentino wanakuwa washindi wa saba tangu kuanza kwa mwaka huu na kuendelea kuwainua vipato watanzania.

“ M-Bet Tanzania itaendelea kuwa nyuma ya mabingwa na mpaka sasa tuna washindi watano ambao wameibuka kuwa mamilionea kupitia mchezo yao,” alisema

Kwa upande wake, Mdimi alisema kuwa ushindi wake umetokana na kuwa makini katika kuchagua timu bila ya kufauata alama za ushindi ambazo kilatimu imekuwa ikipewa katika mkeka.

Alisema kuwa pamoja na ushindi bado klabu ya Arsenal inamoa changamoto sana, hata hivyo, safari hii haikuwepo katika mkeka ambao yeye alibashiri.

“Siri kubwa ya kushinda bahati nasibu hii kujua uwezo wa timu pamoja na kufanyia utafiti wa timu, aina ya wachezaji ambao wamesajili, aina ya timu unayocheza nayo pamoja na majeruhi,” alisema Mdimi.

Ngolle alisema kuwa amefarijika sana na ushindi huu kwani utamfanya kufungua biashara ili kujiongezea kipato.

“Nilikuwa nabashiri ba kupata fedha kidogo kama Sh200,000 na fedha nyingine kidogo, sijakata tamaa na sasa kufanikiwa kupata fedha ambazo nitafanyia masuala ya maendeleo,” alisema Ngolle.