Home Burudani SUPER D AMSAINISHA DEO SAMWELI KUZIPIGA NA VICENTI MBILINYI APRIL 2 P.T.A...

SUPER D AMSAINISHA DEO SAMWELI KUZIPIGA NA VICENTI MBILINYI APRIL 2 P.T.A SABA SABA

0
Bondia Deo Samweli kushoto akibadilishana mkataba na Promota wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila ‘Super D’ baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga na Vicent Mbilinyi mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A SABASABA siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka

Bondia Deo Samweli akisaini mkataba wa kuzipiga na Vicent Mbilinyi mbele ya promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba
………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu

BONDIA DEO SAMWELI amesaini mkataba wa kuzipiga na Vicenti Mbilinyi mpambano wa raundi kumi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba siku ya Ijumaa Kuu  April 2

Akisaini mkataba uho mbele ya mkurugenzi wa kampuni Tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema kuwa amekuja kufanya kazi hivyo mashabiki waje kwa wingi kwani kazi atakayo ifanya siku hiyo si ya kitoto

aliongeza kwa kuserma kwa sasa anarudi upya katika masumbwi kwani mwishoni mwa mwaka jana alijeruhiwa kidogo hivyo ame mtahadharisha mbilinyi kufanya mazoezi kweli kweli kwani siku hiyo akuto kuwa na msalie mtume

Katika mpambano uho atampiga kipigo cha mwana ukome ambapo mbilinyi ato weza tena kumtaka Deo Samweli warudiane nae tena

Nae Promota wa mpambano uho Super D amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani ya masumbwi ni vitasa kwa kwenda mbele katika mpambano uliopewa jina la ‘No Pain No Gain Fight Nigth’

pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ya mabondia mbalimbali ambapo Jemsi Kibazange atazipiga na Hamidu Kwata wakati kassim ahamdi atazidunda na Gabriel Chola na Ramadhani Migwede atazichapa na Albano Clement na mpambano mwingine wa kutisha utakuwa kati ya Maono Ally kutoka bagamoyo atazipiga na Meshacki Mwankemwa kutoka Mbeya na Abdul Ubaya kutoka Mlandizi atazidunda na Daudi Mwita wa Dar