Home Mchanganyiko CCM YASIFU UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI

CCM YASIFU UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI

0

……………………………………………………………

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Ndugu Yusufu Nannila amesifu utekelezaji ilani ya uchaguzi CCM unaofanywa na viongozi wa Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Ndugu Nannila ameyasema hayo baada ya kutembelea kata za Miuta na Kitama na kujionea miradi ya ujenzi wa madarasa, vyoo na bweni katika shule ya msingi na ya sekondari Kitama.

“Sasa hivi unaona namna hela ya Serikali inavyotumika ipasavyo. Tumeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM kwa miradi ya kata ya Miuta, Kitama na kwingineko. Kazi kubwa imefanyika, hongereni sana viongozi kwa utekelezaji mzuri.” Alisema Ndugu Nannila.

Wakati akikagua Madarasa mapya yaliyojengwa kwa fedha za EP4R Ndugu Nannila alipongeza utaratibu alioukuta shuleni wa Mwanafunzi kutunza meza na kiti hadi anamaliza na kusisitiza samani hizo mpya nazo pia zitunzwe na zidumu.

Katika ziara hiyo ya kutembelea Madarasa 2, vyoo tundu 6, bweni la Wanafunzi wa kike na kupanda miti katika shule ya sekondari Kitama iliyopo kata ya Miuta na Madarasa 2 yaliyopo shule ya msingi Kitama iliyopo kata ya Kitama, Ndugu Nannila aliambatana na kamati ya siasa Mkoa wa Mtwara na kupokelewa na Mwenyekiti CCM Wilaya, Mbunge wa Tandahimba Mhe. Katani A. Katani, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Baisa Baisa, Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri.