Home Michezo YANGA YACHAPWA BAO 1-0 DHIDI YA AFRICAN SPORTS MECHI YA KIRAFIKI

YANGA YACHAPWA BAO 1-0 DHIDI YA AFRICAN SPORTS MECHI YA KIRAFIKI

0

******************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Yanga imepoteza bao 1-0 katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya African Sports ya Jijini Tanga inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Timu zote mbili ziliamua kucheza mchezo huo kwaajili ya kujiweka tayari kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi.

Kipindi cha pili timu zote zilitoka bila kufungana ingawa Yanga ilionekana kulisakama sana lango la timu ya African Sport.

Afican Sports ilicheza mchezo wa kuvizia na kuusoma mchezo unaochezwa na wachezaji wa Yanga ndipo wakatumia madhaifu yao kupata bao la kuongoza na la ushindi.