Home Mchanganyiko WANAHABARI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA MRADI WA KAIZEN KUELEKA...

WANAHABARI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA MRADI WA KAIZEN KUELEKA SIKU NYA KILELE CHA KAIZEN NCHINI

0

Mratibu wa KAIZEN Tanzania Bi.Jane Lyatuu akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya utoaji elimu kuhusu mradi wa KAIZEN unaosimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha CBE Jijini Dar es Salaam

Afisa Ufundi wa KAIZEN Bw.Richard Benaya akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya utoaji elimu kuhusu mradi wa KAIZEN unaosimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha CBE Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo ya mradi wa KAIZEN unaosimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Jijini Dar es Salaam.

********************************************

Wanahabari wametakiwa kuendelea kutoa taarifa za umuhimu wa mradi wa KAIZEN na kutangaza shughuli na fursa zinazopatikana kutokana na mradi huo kuelekea siku ya kilele cha KAIZEN nchini itakayofanyika Februari 5 mwaka huu.

Ameyasema hayo leo Mratibu wa Mradi wa KAIZEN nchini Bi.Jane Lyatuu akitoa mafunzo ya mradi huo kwa wandishi wa habari katika ukumbi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mafunzo hayo Bi.Jane amesema lengo la mafunzo hayo ni pamoja na kubwa likiwa ni kuwaelimisha waandishi kuhusiana na mradi huu pia kutangaza shughuli na fursa zinazopatikana kutokana na mradi huu kuelekea siku ya kilele cha KAIZEN nchini itakayofanyika tarehe 5 Februari, 2021 katika ukumbi wa LAPF Kijitonyama jijini Dar es saalam.

Siku ya KAIZEN itatanguliwa na Mashindano ya KAIZEN ambayo yanatarajiwa kufanyika siku ya Tarehe 4 Februari, 2021. Viwanda vya Tanzania vilivyotekeleza KAIZEN kwa ubora na mafanikio katika Nyanja mbalimbali ambapo washindi watapewa zawadi na mgeni rasmi siku ya maadhimisho ya KAIZEN tarehe 5 Februari, 2021 katika ukumbi wa LAPF.