Home Burudani ZAIDI YA WASANII 70 KUTUMBUIZA KWENYE JUKWAA LA SERENGETI MUSIC FESTIVAL DODOMA

ZAIDI YA WASANII 70 KUTUMBUIZA KWENYE JUKWAA LA SERENGETI MUSIC FESTIVAL DODOMA

0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 31,2021 jijini Dodoma wakati akitangaza kuwa zaidi ya wasanii 70 watakiwasha Serengeti Music Festival uwanja wa Jamhuri Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma

Historia itaandikwa kwa mara ya kwanza jiji la Dodoma kuwashuhudia Kwa mara ya  wasanii zaidi ya 70  wanatarajia kutoa burudani katika jukwaa moja katika tamasha kubwa la (Serengeti Music Festival) lililoandaliwa na Serikali kwa lengo la kutangaza sekta ya utalii hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Januari 31,2021 jijini Dodoma na  Katibu Mkuu Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas amesema tamasha hilo ni juhudi za Serikali katika kukuza sanaa na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana hapa nchini.

“Serikali inafanya kazi kubwa sana hasa katika miradi mikubwa ya kimkakati, wakati miradi inatekelezwa kazi na dawa tumeandaa tamasha kubwa barani Afrika pengine na Duniani wasanii zaidi ya sabini wakubwa kupaform katika jukwaa moja” amesema Dkt Abbas.

Amesema kuelekea katika tamasha hilo kubwa litakalofanyika February 6, 2021 litaambatana na matukio mbalimbali kuanzia Februry 1, 2021 hadi kufikia siku ya kilele katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Amesema February 4, 2020 kutakuwa na kongamano kubwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa Mkoa wa Dodoma kukutana na watu maarufu hapa nchini katika nyanja za burudani na siasa kuwapitisha katika njia walizopita hadi kufika walipo sasa.

“Wanafunzi wa vyuo vikuu hapa Dodoma kukutana na role modal wao katika sanaa na siasa watakuwepo watu maarufu watawapitisha njia walizopita hadi sasa wapo hivyo katika mziki, au siasa kila star ataeleza njia alizopita” amesema.

Pia kuelekea katika kilele cha tamasha hilo amesema kutakuwa na mpambano mkali na wa kusisimua wa mechi ya mpira wa miguu  kati ya Bajaj na Boda boda , pia mtanange kati ya Wabunge na wasanii wa bongo flava na mechi ya watani wa jadi wa Simba na Yanga kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma.

Dkt Abbas meongeza kuwa ” siku ya tarehe 5 kutakuwa na Pre Party Loyal ambapo wasanii wakubwa watapaform  ikiwa ni maandalizi ya kuelekea siku yenyewe ya tarehe 6 Jamhuri” amesema.

Amesema katika tamasha hilo pia wasanii waliochika nafasi 4 za juu katika shindano la kutafuta vipaji la bongo star search BSS pia wataburudisha katika tamasha hilo kubwa hapa nchini.

Amesema pia katika tamasha hilo litawapambanisha wasanii wa zamani ambao aidha waliacha mziki na kufanya kazi nyingine na makundi  maarufu ya mziki ya zamani kama East Coast na TMK wanaume, sambamba na na DJ maarufu wa zamani na wa Sasa.