Home Michezo AL HILAL YAICHAPA 2-1 TP MAZEMBE MICHUANO YA SIMBA SUPER CUP

AL HILAL YAICHAPA 2-1 TP MAZEMBE MICHUANO YA SIMBA SUPER CUP

0

TIMU ya Al Hilal ya Sudan imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa michuano maalum ya Simba Super Cup  Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Al Hilal iliyochapwa 4-1 na wenyeji, Simba SC katika mchezo wa kwanza juzi, yamefungwa na Bonganga Vinny dakika ya 30 na Mohamed Musa dakika ya 90 baada ya TP Mazembe kutangulia kwa bao la Moustapha Kouyate dakika ya 12.
Michuano hiyo itakamilishwa Jumapili kwa mchezo kati ya wenyeji, Simba SC na TP Mazembe.