Home Mchanganyiko WAZIRI MWAMBE AKUTANA NA WAZALISHAJI WA SUKARI NCHINI JIJINI DODOMA

WAZIRI MWAMBE AKUTANA NA WAZALISHAJI WA SUKARI NCHINI JIJINI DODOMA

0

  

  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba aliyemtembelea ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akimsikiliza  Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba wakati wa mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba mara baada ya mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

 

Baadhi ya wazalisha wa Sukari Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,wakati wa kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo amesikiliza changamoto zao na kuahidi kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akisisitiza jambo zaidi wakati wa kikao na wazalishaji wa Sukari nchini  pamoja na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Afisa Mtendaji Mkuu Utawala TPC Bw.Jaffari Ally akielezea jambo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe(hayupo pichani) wakati wa kikao cha  wazalishaji wa Sukari nchini ambapo amesikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Prof.Kenneth Bengesi,akizungumza kwenye kikao cha  wazalishaji wa Sukari nchini ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe ameahidi kuzitatua changamoto hizo ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini.

Akizungumza na na wazalishaji hao leo Janauari 29,2021 jijini Dodoma Mhe.Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wenye tija  kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.

”Leo nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia kazi”amesema Mhe.Mwambe.

Hata hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo ili  kuleta maendeleo na kuongeza uzalishaji zaidi nchini .

Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba.