Home Mchanganyiko PINDA ; VIJANA CHANGAMKIENI FURSA ZINAZOTOKANA NA TAFITI ZA WOLDVEG

PINDA ; VIJANA CHANGAMKIENI FURSA ZINAZOTOKANA NA TAFITI ZA WOLDVEG

0
*******************************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda ameitaka vijana kuchangamkia fursa zinazotokana na tafiti  zinazofanywa taasisi ya kimataifa ya mboga duniani(WORLDVEG) Ili kuweza kuwa wazalishaji baada ya mbegu kukamilika na kusaidia jamii   kupata miche kwa urahisi badala ya kuangalia kuzitafuta.

Pinda alitoa rai hiyo baada ya kutembelea kituo hicho ambapo alisema ni fursa moja kubwa kea vijana kujipongeza na kuwa karibu na taasisi hiyo wanaweza kujikuta wanakuwa wazalishaji au kuchukuwa jukumu la kufanya  kile ambacho taasisi inaweza kuwaelekeza na kutoka kwako jamii itaweza kununua miche kea urahisi.
“Miche ya taasisi hii inapatikana Katika mazingira  ya kitafiti hivyo wakiwa katika taasisi hii, kutoka kwako wakulima tutanunua miche kwa urahisi badala ya kuangaika kuzitafuta na wakati mwingine tunakuwa hatuna uhakika nazo lakini hizi ni za uhakika,”Alisema waziri Pinda.
Alisema pia ameomaba vijana wanao soma  katika taasisi za kitafiti kilimo Katika mafunzo wanayopata wasiishie tu kuwapa nadharia za mambo ya kilimo na kuwaeleza jinsi tafiti zilivyofanya ila wawaongezee elimu ya namna ya kuziona fursa hizo na wao wenyewe kuzitumia na bila kusubiri ajira.
“Serikali imewasomesha lakini hajaahidi kuwapa ajira kwani wakishapata elimu na maarifa na wakaona hizi fursa zilizopo hapa kilichobaki ni kujiongeza Ila wanatakiwa kupewa elimu kwanza yenye sura ya ujasiriamali unaolenga kwenye sekta ya kilimo na baada ya hapo tutafanikiwa na kuaanza kukuliza tulichelewa wapi na ni kwanini hatukuwahi mapema kwasababu sekta hii ya mboga matunda na viungo inakuwa kea haraka,” Alisema.
Alieleza kuwa Kama watafanikiwa kuendeleza taasisi hiyo  itakuwa mkombozi kwani wamejikita Katika kujaribu na kuona namna ya kuendeleza na kukuza mbegu za asili ya kiafrika ambazo zipo hapo nchini ambapo sehemu kubwa Zina virutubisho bora zaidi kuliko mboga zinazotoka nje ya Afrika.
“Nimetembea nimeona kazi wanayoifanya, nimeona aina mbalimbali za mazao ambayo wanaotesha kwaajili ya kukuza na kuendeleza kuzalisha aina flani flani za mbegu jambo ambalo limenivutia Sana kwaiyo ombi langu kea serikali ni taasisi Kama hizi ni vizuri sijapewa nafasi kubwa kibajeti,” Alisema waziri Pinda.
Amefanya kuwa serikali ivipe nafasi kubwa kibajeti taasisi hizo kwasababu maendeleo yoyote bila kujiongeza kwa ngufu Katika utafiti wanaweza kukuta wanakwenda lakini wanakwenda gizani ambapo hapo ukienda ndio unaona wanakufua macho ambapo pia alisema katika ilani ya chama cha mapinduzi 2020/2025 ameona Kuna maeneo mengi yanayozungumzia uimarishaji na uendelezaji wa taasisi za utafiti.
Alifafanua nua kuwa tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zinawanufaisha wananchi kwani kwani wanapopata mbegu wanachunguza na kuona mbegu hiyo inaweza kuota Katika maeneo yapi, masharti yake yapoje kwenye udongo, maji na hali ya hewa na kwenda mbali zaidi kwa kuangalia mmea huo una virutubisho gani na kwa kufanya hivyo wanafanya vizuri kwani wanawasaidia wananchi kiuchumi na kiafya lakini pia wajikite Katika kutoa elimu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt Gabriel Rugelema alisema kuwa  sababu kubwa ya kuwa na benki ya mbegu ni kujaribu kutengeneza mbegu bora za kiafrika na kuweza kujitosheleza taratibu ambapo sasaivi wapo katika asilimia 5 huku asilimia 95 kila mkulima anaponunua mbegu anapeleka fedha nje na kuendelea kuwa mtegemezi wa kiuchumi.