Home Michezo TAIFA STARS YAICHAPA 1-0 NAMIBIA YATIA MATUMAINI FAINALI ZA CHAN CAMEROON 2021

TAIFA STARS YAICHAPA 1-0 NAMIBIA YATIA MATUMAINI FAINALI ZA CHAN CAMEROON 2021

0

BAO pekee la Farid Mussa Malik dakika ya 65 limetosha kuipa Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Namibia katika mchezo wa Kundi D Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN). 
Kwa ushindi huo, Tanzania inafufua matumaini ya kwenda Robo Fainali iwapo itashinda mechi ya mwisho dhidi ya Guinea Jumatano.
Baada ya sare ya 1-1 katika michezo uliotangulia leo jioni, sasa Guinea na Zambia zinalingana kwa pointi, nne kila timu zikifuatiwa na Tanzania yenye pointi tatu, wakati Namibia imeaga mashindano baada ya kufungwa mechi zote mbili za mwanzo.