Home Mchanganyiko ASKARI WA KITUO CHA POLISI WILAYANI KIBAHA AKUTWA AMEFARIKI BAADA YA KUJINYONGA...

ASKARI WA KITUO CHA POLISI WILAYANI KIBAHA AKUTWA AMEFARIKI BAADA YA KUJINYONGA NYUMBANI KWAKE

0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hawapo pichani kuhusiana na tukio hilo.

ASKARI wa jeshi la   Polisi Mkoa wa Pwani   mwenye  namba   E 6472   Yusuph Said  (52) ambaye ni mkazi wa Wilayani Kibaha aliyejinyonga  katika  nyumba yake aliyokuwa anaijenga katika maeneo ya kata ya Kongowe hadi kupoteza maisha  akiwa katika picha ya pamoja na askari wenzake  enzi za uwahi wake .(PICHA NA MAKTABA)  

…………………………………………………………………………………….

NA VICTOR MASANGU, PWANI

ASKARI wa jeshi la   Polisi aliyekuwa anafanya kazi katika kituo cha Polisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani  namba   E 6472    Yusuph Said   mwenye umri wa miaka (52)  amekutwa  amejinyonga hadi kufariki dunia  katika  nyumba yake anayoijenga katika maeno ya miembe saba   kata ya Kongowe wilaya ya Kibaha.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea katika eneo la Miembe saba B  kata ya Kongowe Wilayani Kibaha ambapo alisema tukio hilo lilitokea Januari 18 majira ya saa 12 jioni.

Kamanda Wankyo alisema Yusuph alikua akitumikia katika kituo c anaishi Picha ya ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.

Kamanda alibainisha kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kwenda kwao Lindi kwa maziko zikiendelea.

Msaidizi wa balozi kwenye eneo hilo Imelda Kitosi alisema akiwa nyumbani alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mtu kujinyonga ndipo akaenda kushuhudia akiwa na baadhi ya majirani.

Imelda alisema alipofika alipofika alielewa na wazazi wa watoto waliokuwa na karibu ya eneo hilo kuwa kuna watoto waliokuwa wanacheza kombolela nje ya nyumba hiyo ambao walisema walisikia mtu anajipiga ndani ya nyumba na walipochungulia wakamkuta tayari yupo chini akiwa na kamba shingoni na walikimbia kwenda kutoa taarifa.

Wazazi hao walipofika katika nyumba hiyo ambayo bado inajengwa walimkuta askari huyo tayari ameshafariki ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa viongozi na kumpigia msaidizi huyo wa balozi.

“Mimi sasa baada ya kupigiwa simu niliingia hapa pamoja na baadhi ya watu waliokuwa karibu tulimkuta yuko kwenye chumba ambacho kilikua kinajengwa kama bafu au choo kamba kaifunga juu na chini kulikua na tofali ambalo baada ya kuhangaika sana mguu mmoja tulikuta kama umepiga goti na mwingine umeegemea tofali huku kamba ikiwa shingoni” alisema

Balozi huyo alieleza kuwa baada ya kushuhudia tukio hilo ndipo walipiga simu Polisi kutoa taarifa na walifika na kuchukua mwili wa marehemu.