Home Mchanganyiko MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DODOMA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DODOMA

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo Januari 19,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Vitabu vya Mkakati na Muongozo wa kufundishia Lugha ya Kiswahili kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili yaliyoadhimishwa leo Januari 19,2021 katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi, Wajumbe, Wadhamini na Wafanyakazi wa  Taasisi za Kiswahili baada ya Kufungua Maadhimisho ya Siku ya kiswahili katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma Leo Januari 19,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Seikali ya Mapinduzi Zanzibar  Mhe. Tabia Maulid Mwita na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Abdalla Ulega baada ya Kufungua Maadhimisho ya Siku ya kiswahili katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma Leo Januari 19,2021.  

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  ametoa Maagizo kwa Wizara ya Wizara ya Habari ,utamaduni Sanaa na Michezo  Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wizara ya Habari Zanzibar  kuhakikisha zinakaaa na wataalam ili   Kiswahili kitumike katika nyaraka mbalimbali za Serikali  ikiwemo hukumu za mahakama.

Mhe.Suluhu ametoa maagizo hayo leo Januari 19,2021 jijini Dodoma katika maadhimisho ya Kiswahili yaliyoanza leo Januari 19 ,2021 na kutarajia kuhitimishwa kesho Januari 20,2021  ambapo pia  ameagiza  kushirikiana na mabaraza ya Kiswahili[BAKITA na BAKIZA]na kuja na mikakati ya pamoja  katika kukuza Kiswahili kwa kuandaa wataalam wa Kiswahili.

Aidha,Makamu huyo wa Rais amesema Taasisi za kuendeleza lugha ya Kiswahili [BAKITA na BAKIZA] ni muhimu  kukumbukwa  kwa kupatiwa fedha  huku akitoa msisitizo kwa sekta binafsi  kuchapisha machapisho ya Kiswahili.

Pia,Mhe.Suluhu amebainisha kuwa Mapinduzi ya viwanda yatumike katika mfumo wa Kiswahili hususan kwenye mfumo wa kidijitali[TEHAMA].

Hata hivyo Mhe.Suluhu amesema  Kiswahili kinaiunganisha Tanzania  na mataifa mbalimbali katika kukuza uchumi wa nchi na uhusiano mzuri wa kimataifa ambapo ni jambo la kujivunia   huku tafiti mbalimbali zimekuwa zikifanyika na kubainisha kuwa zaidi ya watu milioni 100  hadi 150  duniani wanatumia lugha ya Kiswahili  vyombo vya Habari vikitajwa kuwa na mchango mkubwa katika kueneza Kiswahili.

Makamu huyo wa Rais ameendelea kufafanua kuwa Licha ya mafanikio ya Kiswahili bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitabu vya kufundishia wageni,upungufu wa wataalam wa kufundisha Kiswahili kwa wageni.

Kwa upande wake  Naibu Waziri Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo  Abdallah Ulega amesema Wizara  imeandaa Kanzi  data ya wataalam wa Kiswahili ambapo hadi sasa kuna jumla ya Wataalam 1308  wapo katika kukiendeleza na kukikuza Kiswahili.

Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Taifa [BAKITA ]Dkt.Mathew Samwel amesema tuzo zitakazotelewa katika maadhimisho haya ni pamoja na tuzo kwa mwandishi wa vitabu vingi vya Kiswahili,Mwanafunzi bora ,vyombo vya Habari vinavyofanya vizuri katika lugha ya Kiswahili  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kutunukiwa nishani ya juu ya Shaban Robert  kwa kuendeleza Kiswahili.

Chimbuko la Maadhimisho ya Kiswahili Tanzania ni tarehe 31,Julai,1992  kijiji cha Kwembe Jijini Dar Es Salaam   ili kuendeleza lugha adhimu ya Kiswahili  ambapo kwa mwaka huu yanakwenda sambamba na kaulimbiu isemayo  bidhaisha Kiswahili kwa maendeleo Endelevu ya Tanzania.