Home Mchanganyiko KUNAMBI AFIKA KWENYE SHULE ILIYOHARIBIKIWA NA VYOO, ATOA SH MILIONI 1.5 NA...

KUNAMBI AFIKA KWENYE SHULE ILIYOHARIBIKIWA NA VYOO, ATOA SH MILIONI 1.5 NA MIFUKO 50 YA SARUJI

0

………………………………………………………………………….

TUMUUNGE Mkono Rais Magufuli! Hii ni kauli iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi alipofika katika Shule ya Msingi Ngai iliyopo Kata ya Mchombe ambapo alijionea uharibifu wa Miundombinu ya shule hiyo na kutoa mchango wake.

Akizungumza na viongozi wa Kata ya Mchombe, Walimu wa Shule ya Msingi Ngai pamoja na wanafunzi, Mbunge Kunambi ametoa kiasi cha Sh Milioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo ambavyo vilititia kutokana na mvua kubwa zilizonyeesha.

Kunambi pia ametoa mchango wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa darasa jipya baadae ya kujionea adha wanayopata wanafunzi wa darasa la sita ambao wanasoma kwenye darasa ambalo upande Mmoja wa ukuta umemeguka.

” Ni lazima kama viongozi wa ngazi ya kata na Jimbo tumsaidie kazi Rais Dk John Magufuli, ninajua changamoto wanazokumban nazo watoto wetu kama tutawaacha waendelee kusoma kwenye mazingira ambayo siyo rafiki, ninatoa kiasi hiki cha fedha ili kiweze kuwezesha ujenzi wa vyoo hivi pamoja na hilo darasa moja ambalo watoto wanasoma licha ya kwamba halina upande mmoja wa ukuta,” Amesema Mbunge Kunambi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Aidan Gabriel amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Mbunge Kunambi katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Mlimba huku akimuomba kuendelea kuitupia macho shule hiyo.

” Tunashukuru kwa ujio wa Mbunge wetu, Godwin Kunambi kwa sababu hajaja bure ametuachia mchango wake wa Ujenzi wa vyoo vyetu ambavyo vimetitia, tunampongeza pia kwa moyo wake wa kuchangia ujenzi wa darasa jipya baada ya kuona wadogo zetu wa darasa la sita wakisoma kwenye darasa ambalo liko wazi, sisi tunamuombea kwa Mungu na asichoke kuja kutuona na kutusaidia,” Witness Luoga mwanafunzi wa Darasa la Saba