Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DKT. MWINYI AMELIFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA AMANI ZANZIBAR...

RAIS WA ZANZIBAR DKT. MWINYI AMELIFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA AMANI ZANZIBAR FRIENDS OF ZANZIBAR.

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizindua Kalenda Amani Milele, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la  Amani lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mwakilishi wa Waandishi waliopata Elimu ya Amani Ndg.Abubakar Harith na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar beach resort Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe. Zuberi Ali Maulid, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Sheria,Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe. Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akionesha Kalenda ya Amani Milele baada ya kuizindua katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa Kongamani la Pili la Amani lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort na (kulia kwa Rais) Mwakilishi wa Waandishi wa habari waliopata mafunzo ya Amani Ndg.Abubakar Harith na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)

MUFTI Mkuu wa DRC – Congo Sheikh Abdalla Luamba Mangara akitowa Salamu za Friends of Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar uliofanyika katiuka ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

VIONGOZI wa Serikali wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akilihutubia na kulifungua katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini wa kwanza Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa  na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman.(Picha na Ikulu)

BALOZI wa Norway Nchini Tanzania Mhe.Elisabeth Jacobsen akitowa salamu ya Nchi yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe,Elisabeth Jacobsen akitowa salamu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kongamano la Amani Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Zanzibar na kuandaliwa na Friends of Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)WAJUMBE wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Zanzibar.(Picha na Ikulu)