Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza Mkuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kilichofanyika Jijini Dodoma tarehe 14 Januari, 2021.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano huo wakisikiliza kwa makuni hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Ndg. Tumaini Nyamhokya (kushoto) akieleza jambo wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Mkutano Royal Hoteli Jijini Dodoma tarehe 14 Januari, 2021.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akifurahia jambo pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Ndg. Tumaini Nyamhokya (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa TALGWU, Bw. Rashid Mtima.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Bw. Rashid Mtima (kushoto) akieleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Kaimu Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi, Bi. Pendo Berege (katikati) akiwalimu wajumbe wa kikao hicho salamu maarufu ya mshikamano wa wafanyakazi “Solidarity Forever” wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Ndg. Tumaini Nyamhokya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mara tu baada ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
OWM – KVAU
……………………………………………………………………………
Serikali imetoa maagizo kwa Taasisi na Halmashauri zisizo na mabaraza hai ya wafanyakazi kuunda haraka mabaraza ya wafanyakazi ili mabaraza hayo yaweze kutekeleza sera ya ushirikishwaji mahala pa kazi.
Maagizo hayo yametolewa jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akifungua kikao cha Baraza Mkuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).
Mhe.Mhagama amesema kuwa Mabaraza ya Wafanyakazi ni chombo muhimu na ni chachu ya mahusiano mazuri baina ya waajiri na wafanyakazi katika maeneo ya kazi, pia ni moja ya nguzo kuu katika ushirikishwaji wa wafanyakazi.
“Zipo baadhi ya Halmashauri na baadhi ya Taasisi ambazo hazifanyi vikao vya mabaraza ya wafanyakazi ipasavyo na Halmashauri nyingine hazijahuisha Mabaraza ambayo muda wake umeisha,” amesema Mhagama
Aidha Mhangama a,eeleza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2020 jumla ya Halmashauri 185 kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ni Mabaraza 123 tu ndio yapo hai, huku Mabaraza ya 62 hayapo hai.
”Hivyo nichukue fursa hii kuziagiza Halmashauri husika kuunda Mabaraza hayo na kukaa vikao vya mabaraza kwa Mujibu wa Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali na kuhuisha mabaraza hayo,”amesisitiza
Hata hivyo ameongeza kuwa Taasisi zote ambazo hazijaunda mabaraza na ambazo zimeunda kuhuisha mikataba ya mabaraza hayo na kukaa vikao. Pia amezitaka Taasisi kutenga bajeti ya utekelezaji wa shughuli za mabaraza kutokana na umuhimu wa mabaraza haya katika ulimwengu wa kazi.
Mhangama ameelezea kuwa Serikali inatambua umuhimu wa Vyama Vya wafanyakazi katika kusaidia Waajiri na Serikali kwenye kuboresha mazingira ya kazi kwa ujumla.
“Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika kutekeleza shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuiletea nchi yetu maendeleo,” amesema Mhagama
Pia, Mhe. Mhagama alitumia fursa hiyo kukipongeza Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) pamoja na viongozi wa chama hicho kwa kukamilisha ujenzi wa jengo lao binafsi na kununua magari ambayo yatasaidia utekelezaji wa shughuli za chama.
“Hii ni ishara inayoonesha chama chenu kinaendelea kukua kiuchumi na yote hayao yanawezekana kutokana na nidhamu ya matumizi za fedha, uongozi bora na uwajibikaji,” amesema
Aidha, amewakumbusha Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini kuzingatia falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuendelea kujenga uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira ya utulivu na amani.
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Ndg. Tumaini Nyamhokya alisema kuwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa pamoja na majukumu makubwa waliyonayo wataendelea kuungana na Serikali katika kutatua kero za wananchi kwa kutoa huduma bora wakiongozwa na sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kazi. Sambamba na hayo waliipongeza pia Serikali kwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi.