Home Michezo YANGA YAMNASA BEKI WA TAIFA STARS ASAINI MIAKA MIWILI

YANGA YAMNASA BEKI WA TAIFA STARS ASAINI MIAKA MIWILI

0

Mabingwa wa kihistoria Ligi Kuu Tanzania bara wamezidi kujiimarisha baada ya kunasa saini ya beki  chipukizi wa Klabu ya Mtibwa Sugar Dickson Job ambaye amesaini  mkataba wa miaka miwili .

Chini ya Kocha Mkuu Cedrick Kaze ambaye ameendelea kukiboresha kikosi hicho ambacho kinaongoza msimamo wa Ligi Kuu huku kikiwa hakijapoteza hata mechi mmoja.

Job anaungana na rafiki yake Kibwana Shomari ambaye walicheza kwa pamoja katika timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti boys kilichoshiriki michuano ya AFCON 2017 nchini Gabon ambaye naye alijiunga na Yanga mwaka jana.

Job kwa sasa  yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Cong, kesho katika uwanja wa  Mkapa.