Home Mchanganyiko WAZIRI CHAMURIHO AWATAKA WAFANYAKAZI KUZINGATIA MIKATABA YA KAZI

WAZIRI CHAMURIHO AWATAKA WAFANYAKAZI KUZINGATIA MIKATABA YA KAZI

0

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Uchukuzi(Hawapo pichani), wakati wa ufunguzi, katika ukumbi wa Benki Kuu, mkoani Mwanza.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Sekta ya Uchukuzi, wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho (hayupo pichani)wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi lililofanyika  katika ukumbi wa benki Kuu, Mkoani  Mwanza.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na  wajumbe wa baraza la wafanyakazi la sekta ya Uchukuzi ,mara baada ya kulifungua Mkoani Mwanza.

************************************************

Waziri wa ujenzi na Uchukuzi,  Mhandisi  Leonard Chamuriho  amewataka wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi kuhakikisha wanatekeleza makubaliano yaliyosainiwa kati yao na wakuu wa taasisi ili kuwe na ufanisi na thamani ya fedha.

Waziri Chamuriho ameyasema hayo mara baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa sekta hiyo, lilifanyika katika ukumbi wa chuo cha Benki Kuu (B.o.T) Mkoani Mwanza na kusisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa mtumishi atakayekiuka makubaliano hayo.

“Hatutasita kuchukua hatua pale tutakapobaini kuwa kazi zinafanywa kwa mazoea na kusahau malengo tuliyojiwekea kwa utendaji wa kazi za kila siku. “alisema waziri Chamuriho.

Aidha waziri chamuriho amesisitiza umuhimu wa taasisi za sekta ya uchukuzi kushirikiana ili kuwa na matokeo chanya hususani katika miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa kwenye miundombinu.

Hata hivyo waziri Chamuriho ameeleza changamoto ya vishiria vya uwepo rushwa na kuwataka watumishi wa sekta ya uchukuzi kujiepusha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi.

“Zipo rushwa za aina nyingi, ikiwemo za kuomba fedha, zawadi, mapenzi  na hata kuwanyima haki watu haki zao, unyanyasaji wa kijinsia, na  ukiukaji wa haki za binadamu “. Alisema Waziri Chamuriho.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Gabriel Migire amemuhakikishia Waziri Mhandisi Chamuriho kuwa maelekezo yote yatafanyiwa kazi na kutoa mrejesho kwa kuzingatia

Katika hatua nyingine Mwenyekiti, Gabriel Migire amempongeza Waziri Chamuriho kwa utendaji uliotoa matokea chanya kwenye miradi ya ki  mkakati ya sekta ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Ununuzi na Ukarabati wa Meli za Mv Viktoria na Butiama, ujenzi wa Chelezo, Ujenzi wa Meli Mpya ya MV. Mwanza na Ununuzi wa Ndege.