Home Mchanganyiko KUNAMBI ACHANGIA SH MILIONI 1.5 NA MIFUKO 30 YA SARUJI UJENZI SOKO...

KUNAMBI ACHANGIA SH MILIONI 1.5 NA MIFUKO 30 YA SARUJI UJENZI SOKO LA CHITA

0

…………………………………………………………………..
MBUNGE wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi amemaliza changamoto ya Umeme, Maji na Choo katika Soko la Chita jimboni humo baada ya kutoa Sh Milioni 1.5 , mifuko 30 ya saruji ili kusaidia ukarabati wa soko hilo lengo ni kuwafanya wajasiriamali wa soko hilo kufanya biashara zao vizuri.

Akizungumza sokoni hapo Kunambi pia amempigia simu Meneja wa Tanesco Wilaya ya Mlimba kujua ni lini soko hilo litafungiwa umeme ikiwa ni baada ya kusikia kero ya wananchi hao wakilalamika kutofungiwa umeme licha ya kuwa tayari washalipia gharama zote zinazotakiwa.

Baada ya malalamiko hayo Kunambi alimpigia simu Meneja wa Tanesco mbele ya wananchi hao ambapo Meneja huyo alikiri kuchelewa kufungiwa umeme kwa wananchi hao sokoni hapo na kuahidi kushughulikia changamoto hiyo ndani ya siku chache.

” Leo nimefanya ziara yangu katika kata za Chita, Ching’anda na Chisona, nimetoa mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Udagaji, mifuko 150 kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kata ya Ching’anda lakini Mtendaji wa Kata ndani ya wiki hii ntakua nimeingiza Sh Milioni 2 za kusaidia ukarabati wa ofisi ya walimu hapa Sekondari ya Ching’anda pamoja na vyoo vya wanafunzi, changamoto ya mashine ya vipimo pale Zahanati ntashirikiana na Halmashauri tuilete hapa.

” Nimepita kata ya Chisona hawana kituo cha kusimama Treni, hili nalichukua ntawasiliana na mamlaka husika watuletee kituo hiko hapa, katika kata hiyo pia nachangia mifuko 40 ya saruji, 30 iende Sekondari ya Chisano na 10 ifanyie ukarabati Soko la Chisano,” Amesema Mbunge Kunambi.

Mbunge Kunambi tayari ameshafanya ziara ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa jimbo lake kwenye kata 10 huku akiendelea na ziara zake katika kata sita zilizobaki.