Baadhi ya Viongozi wa dini ya kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja Mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi wa Twariqa mkoani Arusha
Mbunge wa Jimbo la Kijini visiwani Zanzibar mwenye koti Jeusi Yahya Ali maarufu Kama Maambaless,akiwa na Makamu wa Chama Cha NCCR Mageuzi Taifa bw.Ambar Khamis Haji pamoja na Msemaji mkuu wa taasisi ya Twariqa Tanzania Haruna Hussein katika Ziara Yao ya kidini mkoani Arusha.
************************************************
Na.Mwandishi Wetu,Arusha.
Watanzania wametakiwa kuendelea kutenda mema na kuhakikisha kuwa wanakuwa wamoja katika kuandaa vijana kwa ajili ya kuwa viongozi Bora wa Taifa la baadaye.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkoani Arusha katika Mara baada ya kufanya ziara ya kidini,Aliyekuwa Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha NCCR Mageuzi na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho taifa,bw.Ambar Khamis Haji alisema kuwa nyumba za Ibada zikitumika vizuri zitaweza kusaidia kuwa na vijana na Viongozi waaminifu pindi wanapokuwa vijana.
Alisema kuwa kila mwananchi anafaa kufuata maadili mema kwa kuwa vitabu vya dini vinasema kila unapotenda mema basi utalipwa mema.
“Tuendeleeee kushirkiana Kama viongozi wetu wa Taifa wanavyoendeleza mashirikiano bila kujali mipaka lengo liwe ni maendeleo tu haswa katika nyanja hii ya dini kwa kuwa nyumba kama hizi zinasaidia sana, kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mema na tunapata viongozi wazuri hivyo tutaendelea kuboresha ushirikiano na umoja huu”alisema be.Ambar
Nae mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Jimbo la Kijini bw.Yahya Ali Khamis maarufu kama Maambaless alisema kuwa ziara hiyo mkoani Arusha ni mwaliko wa taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa Tanzania ambalo lengo ni kushirikiana katika changamoto mbali mbali na kukuza taasisi hiyo.
Bw.Yahya aliahidi kumalizia ujenzi wa jengo la msikiti wa ngarenaro ambao Ni msikiti mama unaotumiwa na taasisi hiyo pamoja na kununua ardhi kwaajili ya ujenzi wa msikiti na madrasa katika Eneo kata ya Terati.
“Ndugu zangu tuendeleze mashirikiano haya na tusiwe na ubaguzi kama ambavyo wanafanya Marais wetu Dkt.John Pombe Magufuli na dkt.Hussein Mwinyi tuchape kazi bila kujali mipaka mradi tu hatuvunji sheria,penye shida tuitangaze na tusaidiane ili tumalize msikiti huu”alisema bw.Maamballess
Kwa Upande wake sheikh Haruna Hussein ambaye ni msemaji wa taasisi ya Twariqa Tanzania,alisema kuwa ujio huo una maana kubwa kwa taasisi hiyo na daima wataendelea kudumisha Muungano ambao uliasisiwa na Viongozi wa kwanza wa nchi.
Haruna alisema kuwa nia ya Viongozi hao ni kuweza kuhakikisha kuwa wanashirikiana kuleta maendeleo katika mkoa wa Arusha na kuhakikisha kuwa baadhi ya changamoto zinatatuliwa.
Ziara ya kidini kwa Viongozi hao kutoka visiwani Zanzibar,ni kuongeza mashirikiano ya kidini ambapo pia Mbali na kununua Eneo Hilo wameahidi kujenga Msikiti na Madrasa na kutatua changamoto nyingine.