Home Mchanganyiko MCHEZAJI WA TIMU YA MBEGA WEKUNDU FC AFARIKI DUNIA

MCHEZAJI WA TIMU YA MBEGA WEKUNDU FC AFARIKI DUNIA

0

**********************************************

NA DENIS MLOWE, IRINGA
UONGOZI wa Chama Cha Soka Mkoa wa Iringa (IRFA)  umepokea taarifa za Msiba wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya Mbega Wekendu Florian Myinga kwa masikitiko makubwa kilichotekea katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Akizungumza kwa kwa niaba ya IRFA mwenyekiti,Cyprian Kuyava alisema kuwa   wanawapa pole Mbega Wekundu Fc inayoshiriki ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa (Asas Super League 2020) Familia ya Marehemu , Wanafamilia wa soka Wilaya ya Kilolo na Mkoa wa Iringa kwa ujumla wake.
Alisema kitendo cha kumpoteza kijana aliyekuwa Ana ndoto kubwa za soka kinaumiza sana kutokana na kuondoka akiwa bado mdogo hivyo kwa kuwa Bwana alitoa na Bwana ametwaa apumzike kwa Amani kijana Florian.
Kwa upande wake katibu wa IRFA mkoa wa Iringa, Dk. Ally Ngala licha ya kutoa Pole sana Mbega Wekundu kumpoteza mmoja wa aliyekuwa mchezaji wao msimu uliopita amezitaka timu zitakazocheza mechi za Leo na kesho kusimama kwa dakika moja kumuaga na kumbuka mchezaji huyo.
 “Kwa Heshima yake michezo yote ya leo na kesho tutasimama dk moja kwa kumuaga na kumkumbuka kwa dk moja (Moment of silance).”
Aidha alitoa Rai kwa jamii ya soka kwa Pamoja kupitisha mchango kidogo kama kawaida yetu waswahili hata buku buku tu kuonyesha upendo wetu watanzania pindi tupatapo misiba.
Kwa mujibu ya mmoja ya viongozi wa timu ya Mbega Wekundu,Miraji Kindole alisema kuwa marehemu Florian Myinga amefariki Dunia usiku wa Jana 29/12/2020, mnamo saa nne za usiku, katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Alisema chanzo Cha kifo chake ni kuwa marehemu alijikata kidogo na panga kwenye goti akiwa kazini Hali iliyomlazimu alazwe hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa Hadi kifo chake.
Baadhi ya makocha wa timu zinazoshiriki ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa ya Asas Super League wametoa pole kwa uongozi wa timu Mbega Wekendu kwa familia ya marehemu na wadau wa soka kwa ujumla kutokana na msiba mkubwa wa mchezaji huyo kijana.