*********************************
Mkoa wa Dar es salaam Leo umetoa taarifa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha Kwanza kwa mwaka 2021 ambapo jumla ya watahiniwa 76,430 sawa na 86.94% wamefaulu mtihani huo na kufanya Mkoa huo kuongoza kitaifa.
Akitoa taarifa ya wanafunzi waliochaguliwa, Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Paul Makanza amesema jumla ya wanafunzi 61,504 waliofaulu wamepangiwa kujiunga na kidato Cha Kwanza awamu ya Kwanza na wanafunzi 14,926 waliofaulu watapangiwa shule awamu ya pili.
Aidha Bw. Makanza amesema jumla ya vyumba 299 vinahitajika kujengwa ili kupokea wanafunzi hao ambapo Hadi Sasa vyumba 350 vinaendelea kujengwa Katika Manispaa mbalimbali na vinatarajiwa kukamilika kabla ya February 28 mwaka 2021.
Hata hivyo Makanza amewataka wazazi na walezi kuwapeleka wao kwenye shule walizopangiwa ifikapo January 11 mwakani bila kukosa na kuwataka Wakuu wa shule kuwapokea wanafunzi bila kikwazo chochote hususani michango.