Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya

Barabara ya mkoa huo, Dk. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha Bodi ya Barabara

ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe walipata taarifa za  maendeleo ya

ujenzi wa  barabara  mkoani humo kutoka Tanroad na Tarura  Desemba 16, 2020

jijini Dodoma. 

Dk. Mahenge amezitaka Tarura na Tanroads kuwashirikisha

wananchi wa maeneo  husika kwa kupata maoni na ushauri  wao kabla ya kuanza ujenzi wa barabara na

madaraja katika maeneo yao ili kujenga miradi imara inayozingatia jiongrafia na

historia ya eneo husika.    

 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness

Mgalula akisoma ajenda za kikao hicho.

 

 Spika wa Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job

Ndugai  akitoa hoja kuhusu umuhimu wa

Miji midogo kama Kibaigwa  kutengewa na

Tanroads fedha za ujenzi wa barabara na kupanua maeneo ya kuegesha magari yakiwemo

malori  ili kupanua wigo wa kibiashara na

kuongeza ajira kwa vijana katika eneo hilo. Ndugai pia ni mjumbe wa  bodi hiyo.

 

 Mratibu wa Wakala wa

Barabara vijijini  (TARURA) Mkoa wa

Dodoma, Mhandisi  Lusako Kilembe  akitoa taarifa kwenye kikao hicho kuhusu

mipango ya utekelezaji  ya miradi ya

barabara za  Tarura kufikia hadi Novemba,

2020.

 

 Mhandisi Mwandamizi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Mhandisi

Jacob Mukasa akielezea katika kikao hicho , kuhusu manufaa na namna mfuko  unavyopanga vipaumbele vya kutoa fedha.

 Mhandisi wa Barabara wa Tanroads, Clement Ngirwa akielezea

katika kikao hicho, kuhusu utaratibu wa kupandisha hadhi barabara na majukumu ya

Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara katika Hadhi Stashiki.

Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde akichangia hoja akitaka

uwepo utaratibu wa barabara za jamii nazo kutengea fedha kwa ajili ya

matengenezo.

Mbunge wa Kondoa Vijijini, Dk. Ashatu Kijaji  akichangia hoja wakati wa kikao hicho kwa

kuzitaka Tarura na Tanroads kuwa na watalaamu wenye ueledi ili waweze kujenga

miradi imara kuiiko wanaojenga miradi ya barabara na madaraja dhaifu ambayo

mvua ikinyesha  inabomoka kirahisi.

 Mbunge wa Chemba, Mohamed Monni, akichangia hoja wakati wa

kikao hicho.

 Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, 

Sezaria Makota akichangia hoja wakati wa kikao hicho. Kuhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dk. Fatuma Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda.

Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao hicho

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa

wa Dodoma, Mhandisi Salome Kabunda   akitoa

taarifa kwenye kikao hicho kuhusu mipango ya utekelezaji  ya miradi ya barabara za  Tanroads hadi Novemba, 2020.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba,  ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi hiyo, Sambala

Said