Mwenyekiti wa Bodi ya Ura Sacoss Benedict Wakulyamba akizungumza wakati wa mkutano huo |
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime akizungumza wakati wa mkutano huo |
Sehemu ya washirki kwenye mkutano huo wakifuatilia taarifa mbalimbali kwenye makabrasha yao
Sehemu ya washirki kwenye mkutano huo wakifuatilia taarifa mbalimbali kwenye makabrasha yao
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramdahani Kailima amewashauri viongozi wa Chama cha Ushirika wa kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi Tanzania (URA SACOSS) kufungua milango kuwaruhusu watu ambao sio watumishi wa Jeshi hilo kujiunga na chama hicho cha kuweka na kukopa.
Ushauri huo ulitolewa na Kailima wakati akifungua mkutano mkuu wa 12 wa chama hicho uliofanyika mjini Tanga na kudhuhuriwa viongozi wa matawi ya chama hicho kutoka nchi nzima.
Alisema kwamba alikwisha kutoa ombi hilo mara kwa mara mpaka sasa hajaona mwekeleo wake na ndio maana ameona kutumia fursa hiyo kumuomba mwenyekiti mpya wa wa ushirika huo kuona namna ya kulifikiria suala hilo.
“Mwenyekiti mpya naomba mje na mtazamo mpya kutumia kuwashawisha wajumbe kutoa fursa ya kuingia kwa watu ambao sio watumishi wa Jeshi la Polisi nao waweze kujiunga na Saccos hiyo”Alisema
Aidha pia aliwashauri waone namna ya kuweka vitega uchumi vitakavyowezesha Ura Saccos kuimairisha mtaji wake utawakowezesha kuongeza hisa na akiba na hatimye kuwezesha kupunguza riba za wanachama na kuongeza kiwango cha kukopa hatimaye kukuza uchumi wa wanachama.
“Ndugu zangu wanachama nimepitia agenda za mkutano huo hivyo kupitia fursa hii niwaombe muwe makini wakati mkipitia na kujadili mambo yanayowasilihwa kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha ushirika wenu”Alisema
Naibu Katibu Mkuu huyo aliwaasa viongozi Ura sacoss kufanya kila wanaloweza wawe muunganiko kati ya mafaniko ya ura sacos na ustawi wanachama wa URA Sacoss
“Kama hatutakuwa na muunganiko kati ya mafanikio ya bilioni 73 mafanikio ya mwanachama mmoja mmoja itafikia kipindi wanachama watakata tamaa na kuona chama hakina faida”Alisema
Katika hatua nyengine Naibu Katibu Mkuu huyo aligusia suala la rushwa ambapo alisema suala la rushwa wamekuwa wakilaumiwa nalo kwa kubambia watu kesi.
“ Tunatumia kushawishi au kushiriki au kuomba niwaambie watumishi wenzangu hata vitabu vya dini vinaeleza rushwa ni mbaya hata kwa ustawi wenu na familia pia kwani unaweza kupata kizazi cha ajabu ukashangaa kimetoka wapi”Alisema
“Maana asubuhi unaweza kuchukua rushwa ya mtu ambaye hali yake ni mbaya na umekwenda kununua unga umepeleka nyumbani usiku iwe ni askari wa kike au wa kiume umekula umeshiba halafu usiku mnatafuta mtoto kwa nguvu ya rushwa na atakayeingia tumboni ataaingia kwa nguvu ya rushwa”Alisema
Awali akizungumza wakati wa mkutano huo kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu,Mwenyekiti wa Bodi ya Ura Sacoss Benedict Wakulyamba alisema ushirika huo wa Sacoss ulianzishwa mwaka 2006 kwa madhumuni makubwa matano kujenga tabia miongoni mwa wanachama ya kujiwekea fedha za akiba.
Alisema akiba hiyo wanaiweka kutokana na mishahara yao na mapato ya kila siku yanayotokana na shughuli halali ambazo wanakuwa wakizifanya wakiwa watumishi wa Jeshi la Polisi.
Alisema mkutano huo ni muhimu sana huku akieleza kwamba uanachama wa Sacoss unawasaidia askari kupunguza makali ya maisha kutokana na kuwa na uwezo wa kukopa na kuweka akiba.