***********************************
Makamo wa kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi  Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema  Serikali ya Umoja  wa Kitaifa si kambi ya wanasiasa kupeana nyadhifa navyeo bali ni chombo cha matarajio kwa wazanzibari 
Pia amesema kimeundwa kwa minajili ya kuyafikia maridhiano ya kweli ,kuendeleza umoja na mapatano yatakayoondoa chuki,hasama na mgawanyiko .
  
Amesema  serikali ya umoja wa kitaifa pekee haitaondosha kasoro kwa katiba na sheria bali kinachotakiwa ni kupatikana kwa  muafaka wa kijamii utakaozika hasama, visasi, chuki.
Pia amesema  kuna haja ya kuondosha hali kutoamimiana miongoni mwa viongozi ili kuwaweka pamoja na kuwaanisha wanachi wa zanzibar.
Amesema  ipo haja  ya makusudi ya kuondokana na taaswira hasi ya kuachana na mifarakano badala yake wananchi waishi kwa mapatano na umoja. 
Makamo huyo wa Kwanza wa Rais amesema  ipo haja ya kubaini ni kwanini kila unapofanyika uchaguzi na kumalizika huacha athari aidha  za watu kulalamika ,kususia au kugawanyika .
Amesema ni jukumu la msingi kwa serikali iliopo madarakani la  kuwafanya watu waishi bila kuwekeana mifundo kwenye mioyo yao.
Kwa muktadha huo Maalim seif amesema Act wazalendo kitashirikiana na serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dk Mwinyi kwa matarajio ya kusonga mbele.
Amesema wataendeleza ushirikiano  kwa lengo la kuwaweka pamoja wazanzibari , wapendane , washirikiane na kufanya kazi  kwa kuaminiana.
Hata hivyo  amesema SUK ni chombo cha kusafiria na ili msafiri afike salama mahali anakokwenda njia pekee ni viongozi kuaminiana na wananchi wakoshirikiana .